Moravia (Kicheki na Kislovakia: Morava; Kijerumani: Mähren; Kihungaria: Morvaország; Kipoland:Morawy) ni mkoa wa kihistoria katika mashariki ya Ucheki. Jina limetokana na mto Morava.

Bendera ya Moravia
Moravia katika jamhuri ya Uceki
Bendera ya Moravia[1][2]

Pamoja na Bohemia eneo la Moravia ni sehemu muhimu ya Ucheki ambayo ni nchi iliyoanzishwa mwaka 1993 baada ya Slovakia kutoka katika Chekoslovakia.

Mji mkuu wa Moravia ni mji wa Brno (Kijer.: Brünn).

Moravia ilikaliwa na makabila ya Waslavoni tangu karne ya 6. Katika karne ya tisa milki ya Moravia ilikuwa nchi muhimu zaidi kati ya Waslavoni wa Ulaya. Mwanzo wa karne ya 10 milki hii iliporomoka kutokana na uenezaji wa Ujerumani upande wa magharibi na wa Hungaria upande wa mashariki-kusini. Baadaye watawala wa Bohemia na Moravia waliwaalika Wajerumani kuhamia kwa na kuunda miji na kijiji. Hivyo takriban 1/3 ya wakazi wa Moravia waliongea Kijerumani hadi 1945 wakati wajerumani walifukuzwa katika Chekoslovakia.

Katika karne zilizofuata Moravia ilikuwa chini ya athira ya Poland au Ujerumani ikaendelea kuwa sehemu ya Dola Takatifu la Kiroma na tangu 1526 chini ya utawala wa familia ya Habsburg na baadaye ilitawaliwa kama sehemu ya milki ya Austria.

Wakati wa kupasuliwa kwa Austria-Hungaria mwaka 1918 Moravia ilikuwa sehemu la nchi ya Chekoslovakia na tangu 1993 ya Ucheki.

Jina la Moravia linatumiwa na kanisa la kiprotestanti linalojulikana katika nchi nyingi kama "Kanisa la Moravian".

  1. Svoboda, Zbyšek; Fojtík, Pavel; Exner, Petr; Martykán, Jaroslav (2013). "Odborné vexilologické stanovisko k moravské vlajce". Vexilologie. Zpravodaj České vexilologické společnosti, o.s. č. 169. Brno: Česká vexilologická společnost. pp. 3319, 3320. http://www.moravska-vlajka.eu/dokumenty/vexilologie-169.pdf.
  2. Pícha, František (2013). "Znaky a prapory v kronice Ottokara Štýrského". Vexilologie. Zpravodaj České vexilologické společnosti, o.s. č. 169. Brno: Česká vexilologická společnost. pp. 3320-3324. http://www.moravska-vlajka.eu/dokumenty/vexilologie-169.pdf.