Uprotestanti
Uprotestanti ni aina ya Ukristo iliyotokana na Kanisa Katoliki huko Ulaya Kaskazini katika karne XVI kufuatana na tapo la kidini na la kisiasa maarufu kwa jina la "Matengenezo ya Kiprotestanti". Wahusika wakuu wa tapo hilo ni Martin Luther na Yohane Kalvini.
Asili
Martin Luther, daktari wa teolojia na padri mtawa, alisema kuwa Kanisa linapaswa kurejea kwenye mizizi yake, na kutoa uzito zaidi kwa yale yaliyoandikwa katika, Biblia. Luther alidhani kuwa Kanisa limekwenda mbali na mafundisho ya awali. Alichapisha tasnifu 95 kuhusu njia ya Kanisa Katoliki. Wengine wanasema, alizipigilia kwenye mlango wa kanisa la Wittenberg, lakini wengine wanasema hii si kweli. Tasnifu 95 zilichapishwa mnamo mwaka wa 1516 au 1517. Kwa maneno hayo, yalianza Matengenezo ya Kiprotestanti
== Jina ==. Mwaka 1529, Bunge la Speyer (Ujerumani), kikao cha wakuu wa Ujerumani na miji huru kilipokuwa kikiongea dhidi ya Matengenezo lilikataza tena uenezaji wake katika Dola Takatifu la Kiroma mpaka Mtaguso mkuu utakaporudisha utaratibu ndani ya Kanisa.
Lakini watawala waliomuunga mkono Luther walitoa hati ya pamoja inayoanza na maneno Protestamur, yaani Tunapinga.
Mwaka 1555 Amani ya Augsburg ilipitisha kauli ya kwamba cuius regio, eius religio, yaani kila raia anapaswa kufuata madhehebu ya eneo anamoishi, kadiri ilivyopangwa na mtawala wake, la sivyo ni lazima ahame.
Teolojia
Uprotestanti unagawanyika katika maelfu ya madhehebu tofauti, lakini inawezekana kutambua mambo kadhaa yanayolingana katika hayo yote:
Uenezi
Leo Waprotestanti wote duniani wanakadiriwa kuwa kati ya 800,000,000 na 1,000,000,000.
Tanbihi
Marejeo
- Cook, Martin L. (1991). The Open Circle: Confessional Method in Theology. Minneapolis, Minn.: Fortress Press. xiv, 130 p. N.B.: Discusses the place of Confessions of Faith in Protestant theology, especially in Lutheranism. ISBN 0-8006-2482-3
- Dillenberger, John, and Claude Welch (1988). Protestant Christianity, Interpreted through Its Development. Second ed. New York: Macmillan Publishing Co. ISBN 0-02-329601-1
- McGrath, Alister E. (2007). Christianity's Dangerous Idea. New York: HarperOne.
- Nash, Arnold S., ed. (1951). Protestant Thought in the Twentieth Century: Whence & Whither? New York: Macmillan Co.
- Noll, Mark A. (2011). Protestantism: A Very Short Introduction. Oxford: Oxford University Press.
Viungo vya nje
- "Protestantism" from the 1917 Catholic Encyclopedia
- World Council of Churches World body for mainline protestant churches
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uprotestanti kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |