Mozdahir
Mozdahir (kirefu: Mozdahir International Institute; jina la Kifaransa: Institut Mozdahir International, kifupi: IMI) ni shirika lisilo la kiserikali lililo la kimataifa iliyoko Dakar, Senegal.[1][2] Pia ina matawi katika nchi nyingine za Afrika, kama vile Mali, Ivory Coast, Guinea Bisau, na nyinginezo.[3]
Mozdahir ilianzishwa mnamo 2000 na Cherif Mohamed Aly Aidara, mmoja wa viongozi wakuu wa dini ya Shi'i nchini Senegal.[4] Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali inafanya kazi kwenye miradi ya maendeleo inayohusiana na elimu, afya, kilimo, mazingira, upandaji miti, na nishati ya jua, na imeshirikiana na taasisi nyingine kuu zisizo za kiserikali kama vile Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (World Food Programme).[5][6]
Makao makuu ya Mozdahir iko Dakar, karibu na Chuo Kikuu cha Dakar. Chuo kikuu cha taasisi isiyo ya serikali iliyo Dakar ina maktaba na vifaa vya elimu. Mozdahir pia ina kituo cha redio, ambayo ni kituo pekee cha redio cha Shi'i kinachotangazwa sasa nchini Senegal. Linafanya miradi mingi ya maendeleo katika sehemu ya Casamance Kusini mwa Senegal, na pia katika sehemu mbalimbali za Afrika Magharibi. Shirika linasimamia miradi tofauti ya maendeleo vijijini kama vile uundaji wa mashamba mapya ya ndizi.[7]
Marejeo
hariri- ↑ Chérif Mohamed Aly Aidara, président de Mozdahir International: « L'islam ne peut pas être une religion de violence » Seneweb.
- ↑ Sénégal : 127 jeunes de Vélingara s'informent sur l'islam chiite. Shafaqna.
- ↑ APPEL Chérif Mohamed Ali Aïdara, guide des chiites : «Partout dans le monde, les musulmans sont opprimés» Le Quotidien.
- ↑ Finance Islamique : « C'est un moyen de lutte contre la pauvreté » (Chérif Mohamed Aly Aïdara, Président de l'Institut Mozdahir International) Ilihifadhiwa 1 Februari 2020 kwenye Wayback Machine.. Politique221.
- ↑ Le chiisme au Sénégal Mozdahir Ilihifadhiwa 23 Februari 2020 kwenye Wayback Machine.. Shia Africa.
- ↑ Leichtman, Mara A. 2015. Shi'i Cosmopolitanisms in Africa: Lebanese Migration and Religious Conversion in Senegal. Indiana University Press.
- ↑ Leichtman, Mara A. (2017). The NGO-ization of Shi'i Islam in Senegal: Bridging the Urban-Rural Divide. ECAS7: 7th European Conference on African Studies. Basel, 29 June - 1 July 2017.
Viungo vya nje
hariri- Mozdahir Ilihifadhiwa 8 Mei 2020 kwenye Wayback Machine.