Skolastika wa Nursia

(Elekezwa kutoka Mtakatifu Skolastika)

Skolastica (Nursia, Umbria, Italia, 480 hivi – karibu na Monte Cassino, Lazio, 10 Februari 547) alikuwa dada pacha wa Benedikto wa Nursia.

Mt. Skolastica, alivyochorwa na Andrea Mantegna.

Kama kaka yake anajulikana tu kutoka kitabu Majadiliano cha Gregori Mkuu, tunaposikia alivyofuatana naye katika umonaki akawa abesi wa monasteri ya kike huko Plombariola, kilometa 8 kutoka Monte Cassino. Kutokana na muungano wao na Mungu, walitumia kutwa moja kwa mwaka kumsifu na kushirikishana.

Tangu zamani anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu bikira.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 10 Februari[1].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.