Nabii Baruku
Nabii Baruku mwana wa Neria (kwa Kiebrania ברוך בן נריה) alikuwa mwandishi wa karne ya 6 KK, maarufu kama karani, mwanafunzi na rafiki mpendwa wa nabii Yeremia.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu na madhehebu mbalimbali ya Ukristo.
Maisha
haririKadiri ya Yosefu Flavius, alikuwa sharifu wa Uyahudi, mwana wa Neria na ndugu wa Seraia mwana wa Neria, waziri wa mfalme Zedekia wa Ufalme wa Yuda.[1][2]
Baruku aliandika maneno ya Yeremia alivyoagizwa naye[3] akabaki mwaminifu kwake hata katika dhuluma. Yeremia alipokuwa mafichoni alimtuma kusoma katika Hekalu la Yerusalemu utabiri wa adhabu dhidi ya mfalme Yehoyakimu [4] Huenda kama shukrani kwa kutekeleza agizo hilo gumu, Yeremia alimtabiria mema.[5]
Wote wawili walishuhudia maangamizi ya Yerusalemu (587 KK) wakabaki pamoja baada yake[6][7][8]mpaka walipopelekwa nchini Misri.
Uhusiano huo ulifanya Baruku aheshimiwe sana na vizazi vilivyofuata, hata vitabu viliandikwa kwa jina lake:
- Kitabu cha Baruku au 1 Baruku, ambacho ni kati ya deuterokanoni, vinavyoheshimiwa na Kanisa Katoliki na wengineo kama sehemu ya Biblia ya Kikristo
- 2 Baruku, au Syriac Apocalypse of Baruch
- 3 Baruku, au Greek Apocalypse of Baruch
- 4 Baruku, au Paraleipomena of Jeremiah
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Wright, J. Edward, Baruch ben Neriah: From Biblical Scribe to Apocalyptic Seer (University of South Carolina Press, 2003) ISBN 1-57003-479-6
- Avigad, Nahman, Jerahmeel & Baruch, Biblical Archaeology Review 42.2 (1979). 114-118.
- Shanks, Hershel, Jeremiah's Scribe and Confidant Speaks from a Hoard of Clay Bullae, Biblical Archaeology Review 13.5 (1987) 58-65.
- Shanks, Hershel. Fingerprint of Jeremiah’s Scribe. Biblical Archeology Review 2 (1996): 36-38.
- The Seal of Seraiah, Eretz Israel 14 (1978, Ginsberg festschrift) 86-87.
- Baruku katika Catholic Encyclopedia.
Viungo vya nje
hariri- Prophet Baruch Eastern Orthodox icon and synaxarion
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nabii Baruku kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |