Nadharia ya njama (kwa Kiingereza: conspiration theory) ni masimulizi yanayodai kwamba kundi la watu ("wala njama") wamepatana kwa siri ("kula njama") kufanya mambo haramu au mabaya na kuyaficha mbele ya umma.

Picha hii kwenye noti ya dolar 1 ya Marekani imesababisha nadharia ya kuwa kuundwa kwa Marekani ilikuwa mpango wa siri wa shirika la Illiuminati au Wamasoni.

Nadharia za njama kwa kawaida zina ushahidi mdogo au zinakosa ushahidi wowote. Kuna pia nadharia za njama zinazorejelea matukio halisi lakini kuzieleza kutokana na njama isiyojulikana na watu wengi.

Nadharia nyingi za njama zinadai kwamba matukio fulani ya kihistoria hayakutokea jinsi yanavyoelezwa katika vitabu vya historia bali kufuatana na njama fulani.

Mifano hariri

Nadharia za njama zilizokuwa maarufu katika miaka iliyopita ni pamoja na

Nadharia za njama zilizosababisha majanga hariri

Wakati nadharia za njama zilipolengwa dhidi ya kundi fulani katika jamii ziliweza kusababisha majanga kama mauaji ya kimbari au ya kidini.

Marejeo hariri

  1. Moon Base Clavius is devoted to analyzing the conspiracists' claims and attempting to debunk them
  2. Apollo Lunar Surface Journal, Photos, audio, video and complete communication transcriptions of the six successful landings and Apollo 13
  3. Staff Editors (3 February 2005). "Debunking the 9/11 Myths: Special Report – The World Trade Center", Popular Mechanics. Hearst Communication. Archived from the original on 11 January 2015. Retrieved 24 June 2017.
  4. "Conspiracy theories and secret handshakes: what do we know about Freemasons?", Daily Express. 24 November 2015. Archived from the original on 25 January 2018. Retrieved 29 November 2017.

Viungo vya Nje hariri

 
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: