Illuminati (maana ya Kilatini: "wale walioangazwa") ilikuwa jamii ya siri. Adamu Weishaupt, mwanafalsafa na mwanasheria, alianzisha jamii hiyo mwaka wa 1776.

Ishara ya illuminati
Jicho la Mungu mara nyingi husemekana kuwa ishara ya Illuminati. Linapatikana juu ya piramidi nyuma ya muhuri wa dola ya Marekani, nyuma ya Muhuri Mkuu wa Marekani na nyaraka nyingine rasmi.
Adam Weishaupt (1748–1830), Mwanzilishi wa Illuminati

Mwanzoni, walipinga ushirikina, chuki, ushawishi wa dini juu ya maisha ya umma, na ukiukwaji wa nguvu za serikali. Waliunga mkono elimu kwa wanawake na usawa wa jinsia.

Illuminati pamoja na Freemasonry na vyama vingine vya siri vilipigwa marufuku kwa amri ya Charles Theodore mteule wa Bavaria, kwa kutiwa moyo na Kanisa Katoliki, mnamo 1784, 1785, 1787 na 1790.

Katika miaka iliyofuata, kikundi hicho kilishutumiwa kwa ujumla na wakosoaji wa kihafidhina na wa kidini ambao walidai kwamba Illuminati iliendelea kwa siri na ilihusika na mapinduzi ya nchini Ufaransa.

Wasomi wengi wenye ushawishi mkubwa na wanasiasa walijihesabu kuwa wanachama akiwemo Ferdinand wa Brunswick na mwanadiplomasia Franz Xaver von Zach, ambaye alikuwa mtoa amri wa pili. Wanafasihi kama vile Johann Wolfgang von Goethe na Johann Gottfried Herder na Duke anayetawala Gotha na Weimar walivuwa.

Baadaye yakatokea makundi mengine yaliyotumia jina moja. Hakuna ushahidi kwamba makundi ya sasa yana nguvu au ushawishi mkubwa. Wanajiendeleza kwa kutumia jina la Illuminati ya Bavaria ili kuvutia uanachama.

Kwa matumizi mengine Illuminati imetumiwa wakati wa kuresha mashirika mbalimbali ambayo yanadaiwa kuwa ni mwendelezo wa Illuminati ya asili ya Bavaria. Mashirika hayo mara nyingi yamekuwa yakishutumiwa kwa kula njama za kudhibiti mambo ya ulimwengu, kwa kupanga matukio na kuweka mawakala serikalini na kwenye mashirika ili kupata mamlaka na ushawishi wa kisiasa na kuanzisha mfumo mpya wa ulimwengu. Mtazamo huu wa Illuminati umepata tafsiri katika mitazamo mbalimbali maarufu, ikionekana katika riwaya nyingi, filamu, maonyesho ya televisheni, katuni, na video za muziki.