Wayahudi saba na mama yao
(Elekezwa kutoka Ndugu Wayahudi saba na mama yao)
Wayahudi saba na mama yao (walifariki Antiokia, leo nchini Uturuki, 168-160 KK) ni wafiadini wa karne ya 2 KK wanaojulikana kupitia sura ya 7 ya Kitabu cha pili cha Wamakabayo, ambacho ni kati ya Deuterokanoni, na kupitia vyanzo vingine.
Majina yao hayajulikani kwa hakika, lakini ni wazi kwamba wanasifiwa na Waraka kwa Waebrania pia (11:35)[1].
Chini ya mfalme Antioko Epifane, waliteswa kikatili wakauawa kwa sababu ya kushika kwa imani isiyoshindika sheria ya Bwana ili kufikia uzima wa milele. Mama alishuhudia vifo vya watoto wake wote na kushiriki ushindi wao juu ya mateso kabla ya kuuawa mwenyewe [2].
Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wayahudi saba na mama yao kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |