Negev
Negev ni eneo la kusini mwa Israeli. Ni jangwa ambalo linafunika karibu 60% ya ardhi yote ya Israeli katika mipaka yake ya mwaka 1949, takriban kilomita za mraba 13,000. Ni sehemu kubwa ya Mkoa wa Kusini wa Israel.
Asilimia 10 za wakazi wote wa Israeli wanaishi huko.
Jiografia
haririNegev inapakana na Misri na Ukanda wa Gaza upande wa magharibi, Bonde la Arabah halafu Yordani upande wa mashariki, na upande wa kaskazini mpaka wake ni takriban mstari baina ya mji wa Gaza na Ein Gedi karibu na Bahari ya Chumvi.
Sehemu za kaskazini na magharibi za Negev ni tambarare. Katika kusini kuna milima, mabonde na kasoko mbalimbali. Kasoko iliyo kubwa ni Machtesch Ramon.
Wakati wa mvua katika miezi ya baridi na ya masika, mabonde makavu hujaa maji kwa ghafla na jangwa linafunikwa na maua kwa muda mfupi.
Tabianchi
haririUkavu kwenye Negev na hivyo tabia ya kijangwa inaongezeka jinsi unavyoelekea kusini.
Kaskazini mwa Negev, mvua ya kila mwaka bado ni milimita 350-400. Kiasi hicho cha mvua kinaruhusu uwepo wa misitu iliyopandwa.
Kiasi cha mvua huko Be'er Sheva tayari ni mm 200 kwa mwaka pekee. Eilat kwenye kusini hupokea pekee mm 30 kila mwaka.[1]
Miji
haririMji mkubwa katika Negev ni Be'er Sheva ambao ni pia makao makuu ya mkoa wa kusini ukiwa na wakazi 190,000. Kusini kabisa kuna mji wa Eilat ambayo ni bandari kuu ya nchi kwenye Bahari ya Shamu. Upande wa kusini mashariki mwa Be'er Sheva uko mji wa Dimona penye kituo cha nyuklia.
Wakazi
haririMnamo mwaka 2010 Negev ilikuwa na wakazi 630,000 (sawa na asilimia 8.2 za wakazi wa Israel). Watu 470,000 wa Negev (asilimia 75) ni Wayahudi, na 160,000 (asiliia 25) ni Mabedui Waarabu[2]. Nusu ya Mabedui huishi mjini, nusu nyingine bado wana uhusiano na maisha yao ya kimila ya ufugaji wakikalia vijiji visivyotambuliwa na serikali.
Marejeo
hariri- ↑ "Beersheba, ISR Weather". MSN. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-11-17. Iliwekwa mnamo 2008-01-25.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help); Unknown parameter|https://web.archive.org/web/20071117074301/http://weather.msn.com/local.aspx?wealocations=
ignored (help) - ↑ "A Bedouin welcome - Israel Travel, Ynetnews". Ynetnews.com. 1995-06-20. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-29. Iliwekwa mnamo 2011-10-09.
Tovuti nyingine
hariri- Jalada la Sde Boker la nakala kwenye Negev Ilihifadhiwa 28 Juni 2018 kwenye Wayback Machine.
- Tovuti ya Habari ya Negev ya Israeli Ilihifadhiwa 12 Agosti 2018 kwenye Wayback Machine.
- Picha za Negev Ilihifadhiwa 17 Julai 2012 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Negev kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |