Norbert wa Xanten
Norbert of Xanten (Gennep, Jimbo la Cologne, Dola takatifu la Roma, leo nchini Ujerumani, 1080 - Magdeburg, leo katika Saxony-Anhalt, Ujerumani, 6 Juni 1134) alikuwa mtawa aliyeanzisha shirika la Wakanoni wa Premontree, akawa askofu wa Kanisa Katoliki mwenye maisha magumu aliyelenga tu kuungana na Mungu na kuinjilisha watu, wakiwemo Wakristo na wasio waumini.
Norbert wa Xanten | |
Norbert wa Xanten |
Alitangazwa na Papa Gregori XIII kuwa mtakatifu mwaka 1582.
Maisha
haririNorbert alizaliwa na Eriberto, mtawala wa Gennep, lakini alikulia Xanten, kwenye mto Rhein.
Kisha kupewa daraja ya ushemasi mdogo, Norbert alifanywa mkanoni wa Xanten akahudhuria ikulu ya askofu mkuu wa Cologne, Federiko, halafu ile ya kaisari Henri V, akiwa muungamishi wake.
Mwaka 1115, kama shukrani kwa kunusurika katika hatari kubwa, Norbert alianzisha abasia ya Fürstenberg, aliyoiacha pamoja na mashamba yake mbalimbali kwa askofu mkuu Kononi akajitosa kwenda kuhubiri huko na huko.
Kisha kukubaliwa na Papa Gelasio II, mnamo Novemba 1118 alielekea Ufaransa.
Katika mtaguso wa Reims wa mwezi Oktoba 1119 alimuomba Papa Callixtus II amruhusu tena, lakini alikataliwa, labda kwa sababu ya malalamiko ya wakleri dhidi ya mahubiri yake yaliyolaumu dhambi zao pia.
Basi, askofu wa Laon aliona vema kumpatia makazi na kazi ya kudumu: kuanzisha monasteri na shirika jipya katika jimbo lake, kwenye bonde la Prémontré.
Mapema Norbert alipata wafuasi kutoka nchi mbalimbali: Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji wa leo na hata kutoka Romania ya leo, akianzisha nyumba za kitawa Floreffe, Viviers, Saint-Josse, Ardenne, Cuissy, Laon, Liège, Anvers, Varlar, Kappenberg, Grosswardein na kwingineko.
Nyumba hizo zilifuata kanuni ya Agostino wa Hippo.
Mwanzoni zilipokea hata wanawake katika nyumba za pembeni za zenye ugo, lakini miaza hamsini hivi baada ya kifo chake, hawakupokewa tena.
Norbert aliteuliwa na Papa Honori II kuwa askofu mkuu wa Magdeburg mwaka 1126.
Baada ya uchaguzi wa Papa Inosenti II mwaka 1130, Norbert alimkubali dhidi ya antipapa Anakleto II katika sinodi kubwa ya Oktoba 1130 iliyofanyika Wurzburg.
Miaka ya mwisho akawa kansela na mshauri wa kaisari Lotari III.
Alifariki Magdeburg akazikwa katika abasia ya shirika lake ya huko; ila baadaye masalia yake yalihamishiwa monasteri ya Strahov huko Praha.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Vita sancti Norberti, in Monumenta Germaniae Historica, series scriptores
Viungo vya nje
hariri- The Life and Miracles of St. Norbert Ilihifadhiwa 22 Mei 2015 kwenye Wayback Machine.
- Catholic Encyclopedia: St. Norbert
- Founder Statue in St Peter's Basilica
- Norbert von Xanten (von Prémontré)
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |