Novena
Novena (kutoka neno la Kiitalia "novena" lenye asili katika Kilatini: novem, "tisa") ni mfululizo wa sala au ibada ambazo zinazunguka maombi maalumu ambayo kwa kawaida yanafanywa na Wakristo kwa siku tisa mfululizo[1].
Ingawa kuna aina mbalimbali za novena, lengo lake kuu ni kukuza imani, kujitolea, na kuomba msaada wa kutoka mbinguni katika shida au kwa maombi maalumu kama vile toba na msamaha au kwa ajili ya amani[2][3][4] .
Asili ya desturi hiyo ni siku tisa za sala zilizoshikwa na wafuasi wa Yesu huko Yerusalemu kati ya kupaa kwake mbinguni(siku ya 40 baada ya Pasaka) na Pentekoste (siku ya 50) kama walivyoagizwa naye ili wajiandae kujazwa Roho Mtakatifu waweze kumshuhudia ulimwenguni kote[5][6].
Katika Kanisa Katoliki[7], novena mara nyingi hufanywa kwa heshima ya nafsi mojawapo ya Mungu, Bikira Maria, malaika au mtakatifu fulani[8], lakini maarufu sana ni novena ya Huruma ya Mungu ambayo inaanzia Ijumaa Kuu, yaani siku tisa kabla ya Sikukuu ya Huruma ya Mungu, inayofanyika Jumapili ya Pili ya Pasaka. Wakatoliki wengi hushiriki katika novena hiyo kwa kufanya sala maalumu kila siku kwa siku hizo tisa, wakilenga kukuza huruma na upendo wa Mungu kwa njia ya maombezi ya Bikira Maria.
Tanbihi
hariri- ↑ Schnurr, Dennis (1998). Novena for Justice and Peace. US Catholic Conference Publishers. ku. 1–2. ISBN 978-1-57455-237-9.; Quote: "Novenas are devotional prayers repeated nine successive times for special intentions."
- ↑ Stephen F. Brown; Khaled Anatolios; Martin Palmer (2009). Catholicism & Orthodox Christianity. Infobase Publishing. uk. 140. ISBN 978-1-60413-106-2., Quote: Novena, Roman Catholic devotions consisting of prayers or services held on nine consecutive days or weeks honoring Mary, the mother of Jesus, or the saints
- ↑ Thomas Carson (2003). New Catholic Encyclopedia: Mos-Pat (tol. la 2nd). Thomson/Gale. ku. 465–468. ISBN 978-0-7876-4004-0.
- ↑ Sosa, Juan J. (1982). "Illness and Healing in Hispanic Communities". Liturgy. 2 (2). Routledge: 64–67. doi:10.1080/04580638209408609.
- ↑ Mdo 1:14
- ↑ "Novena for Pentecost: Feast of the Ascension". National Catholic Reporter (kwa Kiingereza). 2020-05-21. Iliwekwa mnamo 2020-06-18.
- ↑ Jonathan H. X. Lee; Kathleen M. Nadeau (2011). Encyclopedia of Asian American Folklore and Folklife. ABC-CLIO. ku. 350–351. ISBN 978-0-313-35066-5.
- ↑ Hilgers, Joseph. "Novena." The Catholic Encyclopedia Vol. 11. New York: Robert Appleton Company, 1911Kigezo:PD-notice
Marejeo
hariri- Barbara Calamari & Sandra DiPasqua, Novena, Penguin Studio, 1999. ISBN 0-670-88444-8.
- Right Reverend Monsignor Joseph F. Stedman, The New Revised 'Triple' Novena Manual, Confraternity of the Precious Blood, 1975.
Marejeo mengine
hariri- William G. Storey (2005). Novenas: Prayers of Intercession and Devotion. Loyola University Press. ISBN 978-0-8294-2161-3.
Viungo vya nje
hariri- List of Novenas at PrayMoreNovenas
- "Novena for the repose of the soul of John Paul II" Archived 2005-12-19 at the Wayback Machine, United States Conference of Catholic Bishops (USCCB)
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Novena kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |