Papa Sixtus II alikuwa Papa kuanzia tarehe 30 Agosti 257 hadi kifodini chake tarehe 6 Agosti 258[1]. Alitokea Ugiriki[2].

Kuuawa kwa Papa Sixtus II na mashemasi wake 6.

Alimfuata Papa Stefano I akafuatwa na Papa Dionysius.

Alirudisha umoja na makanisa ya Mashariki na Afrika Kaskazini uliowahi kuhatarishwa na misimamo tofauti kuhusu ubatizo uliotolewa na waliojitenga na Kanisa Katoliki.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini pamoja na mashemasi wake sita: Januari, Vinsenti, Magnus, Stefano, mbali ya Agapito na Felisisimi waliouawa siku hiyohiyo sehemu nyingine chini ya kaisari Valeriani[3]. Katika Kanuni ya Kirumi anatajwa pamoja na shemasi wake wa saba, Laurenti.

Sikukuu yake ni tarehe 7 Agosti[4].

Tazama pia hariri

Maandishi yake hariri

Tanbihi hariri

  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. (2005) Encyclopaedic Dictionary Of Christian Antiquities (in 9 Volumes) (in en). Concept Publishing Company, 936. ISBN 978-81-7268-111-1. 
  3. Script error: No such module "template wrapper".
  4. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Sixtus II kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.