Pelusius wa Abitina
Pelusius wa Abitina ni jina la mmojawapo katika kundi la Wakristo 49 ambao mwaka 304, wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian, walihukumiwa kwa kuadhimisha Siku ya Bwana huko Abitinae[1][2][3], mji wa Afrika Kaskazini (leo Tunisia).
Tarehe 24 Februari mwaka 303, Diokletian alikuwa ametangaza hati yake ya kwanza dhidi ya Wakristo, akiagiza uteketezaji wa Biblia na maabadi ya Kikristo katika Dola la Roma lote, pamoja na kukataza Wakristo wasikutane kwa ajili ya ibada.[4]
Ingawa Fundanus, askofu wa Abitinae, alikubali kukabidhi maandiko matakatifu ya Kanisa kwa serikali, baadhi ya waamini waliendelea kukutana kwa siri chini ya padri Saturninus. Basi, walikamatwa na kupelekwa na mahakimu wa huko hadi Karthago, makao makuu ya mkoa, kwa ajili ya hukumu.[5]
Tarehe 12 Februari gavana Anullinus alisikiliza kesi. Mmoja wa watuhumiwa, Dativus, alikuwa mjumbe wa senati. Ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhojiwa, kuteswa na hatimaye kufa.[6][7]
Saturninus alifuata na kushika msimamo katika kuteswa. Wote walifanya vilevile, wanaume kwa wanawake wakiwemo watoto wake 4.
Kati ya majibu waliyotoa hao wafiadini, moja limetajwa mara nyingi: Emeritus, aliyekuwa mwenyeji wa wenzake, alipoulizwa kwa nini aliwakaribishwa kwa ibada kinyume cha sheria, alijibu: "Sine dominico non possumus" ("Hatuwezi kuisi bila ya Bwana").
Tangu kale wafiadini hao wote wanaheshimiwa kama watakatifu.
Orodha ya wafiadini wa Abitina
hariri- Saturninus wa Abitina, padri
- Saturninus bin Saturninus
- Felix bin Saturninus
- Maria binti Saturninus
- Hilarion bin Saturninus
- Dativus, mjumbe wa Senati
- Felix mwingine
- Felix mwingine tena
- Emeritus wa Abitina
- Ampelius wa Abitina
- Benignus bin Ampelius
- Rogatianus wa Abitina
- Quintus wa Abitina
- Maximianus au Maximus
- Telica au Tazelita
- Rogatianus mwingine
- Rogatus wa Abitina
- Ianuarius wa Abitina
- Cassianus wa Abitina
- Victorianus wa Abitina
- Vincentius wa Abitina
- Caecilianus wa Abitina
- Restituta wa Abitina
- Prima wa Abitina
- Eva wa Abitina
- Rogatianus mwingine tena
- Givalius
- Rogatus wa Abitina
- Pomponia wa Abitina
- Secunda wa Abitina
- Ianuaria wa Abitina
- Saturnina wa Abitina
- Martinus wa Abitina
- Clautus wa Abitina
- Felix junior
- Margarita wa Abitina
- Maior wa Abitina
- Honorata wa Abitina
- Regiola wa Abitina
- Victorinus wa Abitina
- Pelusius
- Faustus wa Abitina
- Dacianus wa Abitina
- Matrona wa Abitina
- Caecilia wa Abitina
- Victoria, bikira kutoka Karthago
- Berectina wa Abitina
- Secunda mwingine
- Matrona mwingine
- Ianuaria mwingine
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Jean-Yves Congar, Encyclopedia of Christian Theology (Taylor & Francis 2004 ISBN 978-0-20331901-7). vol. 1, p. 499
- ↑ Annuario Pontificio 2013 (Libreria Editrice Vaticana 2013 ISBN 978-88-209-9070-1), p. 822
- ↑ Sancti Aureli Augustini Scripta contra Donatistas, pars I, p. 359
- ↑ Bleckmann, Bruno. "Diocletianus." In Brill's New Pauly, Volume 4, edited by Hubert Cancik and Helmut Schneider, 429–38. Leiden: Brill, 2002. ISBN 90-04-12259-1
- ↑ Santi Martiri di Abitina
- ↑ Dictionary of Christian Biography and Literature to the End of the Sixth Century A.D., with an Account of the Principal Sects and Heresies
- ↑ Dativo e i martiri di Abitina Archived Septemba 1, 2008, at the Wayback Machine
- ↑ Under that date the Roman Martyrology records the names of all forty-nine: Martyrologium Romanum (Libreria Editrice Vaticana, 2001 ISBN 88-209-7210-7)