Umbra

(Elekezwa kutoka Penumbra)

Umbra ni sehemu ya kivuli penye giza zaidi. Inaweza kuitwa pia kitovu cha kivuli.

Kupatwa kwa Jua tar. 29 Machi 2006

Kupita kwa kivuli cha Mwezi duniani wakati wa kupatwa kwa Jua. Watu katika eneo kubwa la giza waliona kupatwa kwa Jua kisehemu. Nukta nyeusi inaonyesha sehemu ya "umbra" ambako Jua lilipatwa kabisa. Duara kubwa zaidi la kijivu linaonyesha maeneo katika "penumbra", yaani kivuli cha kando.
"Central duration" inataja muda wa kupatwa kabisa kwenye kitovu cha kivuli; namba katika kona ya juu huonyesha saa za tarehe 29 Machi kupatwa kulipotokea.
Umbra na penumbra katika kivuli sakafuni kinachosababishwa na milango.

Jina hilo hutumiwa hasa kutaja aina ya kivuli kinachotokea wakati wa kupatwa kwa Jua au kupatwa kwa Mwezi.

Umbra au kitovu cha kivuli hutofautishwa na penumbra au kivuli cha kando, ambako giza linapungua.

Wakati wa kupatwa kwa Jua umbra ni eneo jembamba la kilomita kadhaa ambako Jua linafunikwa kabisa na Mwezi ikiwa giza linatokea kwa dakika kadhaa wakati wa mchana.

Katika sehemu pana zaidi za penumbra au kivuli cha kando, Jua linaonekana kisehemu; karibu na kanda ya umbra mwanga unapungua lakini kwenye sehemu za nje ya penumbra tofauti ya mwanga ni ndogo.

Marejeo hariri

 *[www.astronomy.ohio-state.edu/~pogge/Ast161/Unit2/eclipses.html Pogge, Richard "Lecture 9: Eclipses of the Sun & Moon"], Astronomy 161: An Introduction to Solar System Astronomy. Ohio State University. Imeangaliwa Mei 2021

  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Umbra kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.