Peregrini wa Auxerre

Peregrini wa Auxerre (kwa Kilatini: Peregrinus; alifia dini Bouhy, leo nchini Ufaransa, 304 hivi) alikuwa askofu wa kwanza wa mji huo aliyeuawa kwa kukatwa kichwa kwa ajili ya imani yake wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian[1].

Mapokeo yanasema kwanza alikuwa padri wa Roma aliyetumwa na Papa Sixtus II huko Galia kwa ombi la wananchi, akainjilisha Marseille, Lyon na Auxerre alipoleta wengi kwa Kristo[2].

Hatimaye aliuawa pamoja na padri Marsus, shemasi Kokodomi, shemasi mdogo Joviani na msomaji Joviniani[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Mei[4].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/90598
  2. st_peregrine. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-09-27. Iliwekwa mnamo 2020-05-13.
  3. "Patron Saints Index: Saint Jovinian of Auxerre". Archived from the original on 2012-08-28. Retrieved 2007-07-24
  4. Martyrologium Romanum

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.