Petro wa Anagni (alizaliwa Salerno, Campania - alifariki 3 Agosti 1105) anakumbukwa kama askofu wa mji huo wa Italia ya Kati kwa muda wa miaka 43.

Kabla ya hapo aliishi kama mmonaki kati ya Wabenedikto hadi alipoitwa na kardinali Ildebrando wa Soana kuhamia Roma.

Monasterini aling'aa kwa uaminifu wake katika kushika kanuni, halafu jimboni aling'aa kwa juhudi za kichungaji. Pia alimalizia ujenzi wa kanisa kuu[1].

Papa Paskali II alimtangaza mtakatifu tarehe 4 Juni 1110[2].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake.[3]

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/93385
  2. Vincenzo Fenicchia, BSS, vol. X (1968), col. 663.
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo

hariri
  • Filippo Caraffa e Giuseppe Morelli (curr.), Bibliotheca Sanctorum (BSS), 12 voll., Istituto Giovanni XXIII nella Pontificia Università Lateranense, Roma 1961-1969.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.