Quodvultdeus (jina la Kilatini lenye maana ya "Anachotaka Mungu"; alifariki Napoli, Italia, mwaka 450 hivi) alikuwa Mberberi aliyehudumia kama askofu wa Karthago (katika Tunisia ya leo) tangu mwaka 435 hadi 439 alipofukuzwa na mfalme Genseriki wa Wavandali Waario alipoteka mji huo. Yeye na waklero wake walipandishwa juu ya meli chakavu zisizo na tanga wala makasia, kumbe walifika salama nchini Italia alipohamia hadi kifo chake[2][3].

Mozaiki ya karne ya 5 ya Quodvultdeus, Catacombs of San Gennaro, Napoli[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Februari[4]; lakini pia 8 Januari, 26 Oktoba au 28 Novemba[5].

Maisha hariri

Mwaka 407 alikuwa akiishi Karthago akawa shemasi mwaka 421. Aliongozwa kiroho na Augustino wa Hippo[3] ambaye alimtolea baadhi ya maandishi yake.[3]

Maandishi hariri

 
Ukurasa wa kwanza wa kitabu cha hotuba zake dhidi ya Wayahudi, Wapagani na Waario ambazo kwa muda mrefu zilidhaniwa kuwa za Augustino wa Hippo (Bavarian State Library Clm 14098, f. 61v)

Baadhi ya maandishi yake mwenyewe yametufikia, zikiwemo hotuba 12, kati yake 3 juu ya Kanuni ya Imani (kilichotafsiriwa katika Kiingereza kama The Creedal Homilies: conversion in fifth-century North Africa, Thomas Macy Finn (translation and commentary), New York : Newman Press, 2004, p. 137.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Gillian MacKie, Early Christian Chapels in the West (University of Toronto Press, 2003), 31.
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/41910
  3. 3.0 3.1 3.2 "Patron Saints Index: Saint Quodvultdeus". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-04-05. Iliwekwa mnamo 2019-05-25. 
  4. Martyrologium Romanum
  5. https://catholicsaints.info/saint-quodvultdeus/

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.