Reli ya SGR Tanzania

Reli ya SGR Tanzania au Reli ya geji sanifu ya Tanzania ni mradi wa kuunganisha Tanzania na nchi jirani kwa njia ya reli ya geji sanifu yenye upana wa milimita 1,435. Njia ya geji sanifu inalenga kufika Rwanda na Uganda, na kupitia nchi hizi mbili, hadi Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Reli mpya ya geji sanifu imekusudiwa kuchukua nafasi ya mfumo wa reli ya zamani inayotumia geji ya mita moja.[1] [2] Inaendeshwa na Shirika la Reli Tanzania (TRL).

Mahali

hariri

Mfumo wa reli umepangwa kuwa na sehemu kuu zifuatazo:

Sehemu ya Dar es Salaam-Morogoro

hariri

Sehemu hii yenye urefu wa km 300, ilianza kujengwa kwa ushirikiano wa kampuni ya Yapi Merkezi kutoka Uturuki na ile ya Mota-Engil ya Ureno. Ujenzi ulianza mwezi Aprili 2017 [2] kwa kufadhiliwa kwa njia ya mkopo wa dolar za Marekani bilioni 1.2 kutoka Eximbank ya Uturuki. [3]

Kufikia Februari 2019, asilimia 42 ya kazi kwenye sehemu hii iliripotiwa kukamilika. [4] Mnamo Mei 2019, ilitangazwa kuwa asilimia 60 zilikamilika na kwamba treni za kwanza za abiria zilitarajiwa kuanza huduma mnamo Desemba 2019. Kwenye mwezi wa Oktoba serikali ilitangaza mchakato wa kununua mabehewa ya mizigo 1,430, injinitreni 20 na mabehewa ya abiria 60[5].

Katika Novemba 2019 TRC ilieleza kuwa kazi zimecheleweshwa na mvua ilhali asilimia 70 zimekamilika.

Mpango wa awamu ya kwanza una vituo sita: Dar es Salaam, Pugu, Soga, Ruvu (Kibaha), Ngerengere na Morogoro. Treni tatu zimepangwa kusafiri pande zote kila siku. [6]

Tarehe 14 Juni 2024 treni ya kwanza ilisafiri toka Dar es Salaam hadi Morogoro, tangu saa 12:01 asubuhi hadi 1:55 asubuhi. Ilikuwa na mabehewa 14 na abiria 600-700 hivi.

Sehemu ya Morogoro-Dodoma-Makutopora

hariri

Ushirikiano wa Yapi Merkezi na Mota-Engil ilipewa pia kazi kwa awamu ya pili kutoka Morogoro kupitia Dodoma hadi Makutopora (Manyoni, Singida)[7] kwa urefu wa km 426. [8] Ujenzi huu uangharamiwa kupitia mkopo kutoka Benki ya Standard Chartered wa dolar bilioni 1.46. [3]

Mpango wa awamu la pili una vituo vifuatavyo: Morogoro, Mkata, Kilosa, Kidete, Gulwe, Igunda, Dodoma, Bahi na Makutopora,

Sehemu ya Makutopora-Isaka

hariri

Sehemu hii, yenye urefu wa km 435 kutoka Makutopora kupitia Tabora hadi Isaka bado haijapewa mkandarasi wakati wa Septemba 2018. [3]

Hapa Isaka njia za reli zitagawana; mkono mmoja utaendelea hadi Mwanza ilhali mkkono mwingine unatarajiwa kuendelea hadi mpaka wa Rwanda.

Sehemu ya Isaka-Shinyanga-Mwanza

hariri

Sehemu ya km 220 kutoka Isaka kupitia Shinyanga hadi jiji la Mwanza, kwenye mwambao wa kusini mwa Ziwa Viktoria [9] imepangwa kujengwa na makampuni mawili ya China ambayo ni China Civil Engineering Construction (CCEC) and China Railway Construction Company (CRCC). Mkataba juu ya mradi huo mwenye thamani ya bilioni USD 1.3 ulitiwa sahihi kwenye Januari 2021. Tarehe 14 Juni 2021 rais Samia Suluhu Hassan aliweka jiwe la msingi kwa ujenzi mjini Mwanza. [10]

Sehemu ya Isaka-Rusumo

hariri

Mkono mwingine unapangwa kuendelea kutoka Isaka hadi Rusumo kwenye mpaka wa Rwanda, kwa jumla kuelekea Kigali. Sehemu hii ina urefu wa km 371. Ujenzi wa sehemu hii umekadiriwa kufika dolar milioni 942 za Marekani. [11] Mnamo Aprili 2018, gazeti la EastAfrican liliripoti kwamba Benki ya Dunia imeelezea nia yao ya kufadhili reli ya Isaka-Kigali Standard Gauge. [1]

Reli ya umeme

hariri

Reli hii itatumia nguvu ya umeme kama chanzo cha nishati kwa injini za treni.

Awamu la kwanza Dar es Salaam - Morogoro litategemea kituo cha umeme cha Kinyerezi kinachochoma gesi kwa kuzalisha umeme[12]; umeme utapitishwa kwa waya inayobeba kV 220 kutoka Kinyerezi hadi kituo cha Kingolwira karibu na Morogoro.

Kwa awamu la pili kuna vituo viwili vya umeme vya Tanesco pale Kingolwira na Dodoma vitakavyohudumia mahitaji ya reli. Kituo cha tatu cha kV 220 kitatengenezwa kati ya vituo vilivyopo. Mfumo wote utamilikiwa na Tanesco kwa ajili ya mahitaji ya reli.[13]

Maelezo ya jumla

hariri

Hii njia ya reli yenye geji sanifu ya milimita 1,435 inalenga kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa kati ya bandari ya Dar es Salaam na Kigali, nchini Rwanda, baadaye pia na Bujumbura, nchini Burundi, na hatimaye Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo . Kutoka bandari ya ziwa ya Mwanza, feri za Ziwa Viktoria zinatarajiwa kusafirisha bidhaa kati ya Mwanza na Port Bell karibu na jiji la Kampala, mji mkuu wa Uganda. [14] [15] [16]

Treni za mfumo wa SGR nchini Tanzania zitatumia umeme. [17]

Angalia pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 Olingo, Allan (29 Aprili 2018). "Tanzania turns to World Bank to fund its modern railway project". Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 TanzaniaInvest.com (14 Aprili 2017). "Dar Es Salaam-Morogoro Standard Gauge Railway Works Start". TanzaniaInvest.com. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 3.2 Olingo, Allan (15 Septemba 2018). "Tanzania secures $1.46 billiob SGR loan from Stanchart". Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Nachilongo, Hellen (12 Februari 2019). "Construction of Dar-Moro SGR reaches 42pc". Iliwekwa mnamo 16 Februari 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Tanzania Standard Gauge Railway to Start Operations in December 2019". TanzaniaInvest (kwa American English). 2019-07-10. Iliwekwa mnamo 2019-11-03.
  6. Allan Olingo (11 Mei 2019). "Dar SGR project inches closer to reality as locomotives to test phase one arrive". Iliwekwa mnamo 12 Mei 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Raimund Vogelsberger, Dimitri Militschenko (30 Agosti 2019). "Non-Technical Summary: Environmental and Social Impact Assessment (ESIA) for the Standard Gauge Railway Line (SGR) Project, Dar es Salaam – Makutopora, Tanzania" (PDF). yapimerkezi.com.tr.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: url-status (link)
  8. Xinhua (15 Machi 2018). "Tanzanian president launches construction of new phase of standard gauge railway". Xinhua. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-03. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Globefeed.com (16 Septemba 2018). "Distance between Isaka, Tanzania and Mwanza, Tanzania". Globefeed.com. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. President Samia lays foundation stone for SGR construction project linking lake and inland ports Archived 9 Julai 2021 at the Wayback Machine., Daily News tarehe 14.06.2021
  11. Kabona, Esiara (29 Januari 2018). "Isaka-Kigali SGR works to start in October". Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. Dkt. Kalemani afanya ziara Kinyerezi II na kukabidhiwa mtambo wa kuzalisha umeme kwa njia ya Gesi na mvuke Archived 31 Oktoba 2020 at the Wayback Machine., tovuti ya Tanesco, bila tarehe (iliangaliwa Oktoba 2020)
  13. Non-Technical Summary, Environmental and Social Impact Assessment (ESIA) for the Standard Gauge Railway Line (SGR) Project, Dar es Salaam –Makutopora, Tanzania. 30 August 2019
  14. Barigaba, Julius (27 Juni 2018). "Uganda resumes cargo operations on Lake Victoria after a decade". Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. Tairo, Apolinari (9 Julai 2018). "Tanzania unveils cargo train to Uganda". Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  16. The Citizen Reporter (27 Juni 2018). "Tanzania's MV Umoja resumes Port Bell-Dar route after 10 years". Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  17. Olingo, Allan (18 Machi 2018). "Rwanda, Tanzania agree on electric SGR, opt for open tender". Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

hariri