Renatus Leonard Nkwande

Renatus Leonard Nkwande (alizaliwa Mantare, Tanzania mnamo Novemba 12, 1965) ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza nchini Tanzania tangu Mei 12, 2019.

Maisha

hariri

Nkwande alisoma shule ya msingi huko Sumve. Mnamo 1981 alijiunga na Seminari ya Mt. Maria Nyegezi. Mwaka 1987 alikwenda Seminari kuu ya Kibosho katika Jimbo Katoliki la Moshi na mnamo 1989 alisoma teolojia katika Seminari ya St Charles Lwanga jijini Dar es Salaam.

Mnamo Julai 2, 1995 alipadrishwa kuwa kasisi wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza. Alisoma huko Roma masomo ya Sheria za Kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana kati ya miaka 2002-2005. Hadi kuteuliwa kwake kuwa askofu, alikuwa Kasisi Mkuu na msimamizi wa Jimbo kuu la Mwanza. [1]

Mnamo Novemba 27, 2010 Renatus Leonard Nkwande aliteuliwa kuwa askofu wa Dayosisi mpya ya Bunda. Aliwekwa wakfu kuwa askofu mnamo Februari 20, 2011.

Mnamo Februari 11, 2019, Askofu Nkwande aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza na kuanza tena kazi rasmi mnamo Mei 12, 2019. [2] [3]

Marejeo

hariri
  1. allAfrica.com: Tanzania: First Bishop Appointed to New Diocese of Bunda
  2. https://zenit.org/articles/africa-pope-names-new-leaders-in-three-dioceses/
  3. https://www.vaticannews.va/sw/church/news/2019-05/askofu-mkuu-renatus-leonard-nkwande-jimbo-kuu-mwanza-kusimikwa.html
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.