Romedi (kwa Kilatini: Romedius; kwa Kiitalia San Romedio; 330 hivi - 405 hivi) alikuwa mtoto wa mtemi wa Thaur katika bonde la mto Inn karibu na Innsbruck (Tirol, Austria).

Sanamu yake huko Barco di Sopra (Albiano, Italia)

Hata hivyo, akiwa bado kijana, alijitenga kwenda kutafakari katika pango.

Alipofiwa wazazi wake, aliliachia Kanisa mali yake yote akaenda kushika maisha ya toba katika Val di Non (leo katika mkoa wa Trentino-Alto Adige, Italia). Makao alipoishi hadi leo yanaitwa jina lake.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Januari[1].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.