Ruthu ni mmojawapo kati ya wanawake wachache ambao ni wahusika wakuu wa kitabu kimojawapo cha Biblia, kiasi cha kukipa jina.

Ruthu alivyochorwa na Antonio Cortina Farinós.

Katika fujo ya miaka ya Waamuzi (inayosimuliwa na Kitabu cha Waamuzi), habari ya kitabu hiki kifupi inatujenga: inahusu Ruthu, mwanamke Mpagani wa kabila la Moabu aliyeolewa na Mwisraeli kwao, huko ng’ambo ya mto Yordani.

Baada ya kufiwa mume wake akafuatana na mama mkwe Naomi hadi Bethlehemu ili aolewe na ndugu wa marehemu na kumzalia mtoto kadiri ya Torati, sheria ya Israeli.

Baada ya kufanikiwa kuolewa na Boazi kwa msaada wa Naomi, alimzaa Obedi.

Huyo mtoto akawa baba wa Yese na babu wa mfalme Daudi.

Hivyo kwa uaminifu wake mwanamke huyo pia akatajwa katika Injili kama bibi wa Yesu (Math 1:5-6).

Anaheshimiwa na baadhi ya Wakristo kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Julai.

MazingiraEdit

Habari kuu ya kitabu cha Ruthu ilitokea wakati wa Waamuzi, lakini inafurahisha moyo, ikilinganishwa na hali mbaya ya kidini na ya kimaadili iliyoandikwa katika kitabu cha Waamuzi.

Habari yenyewe inaonyesha kwamba imani kamili kwa Mungu na uangalifu na upendo kwa watu wengine wakati ule pia ulikuwepo katika Israeli.

Katika taifa zima walikuwepo watu waliojitahidi kuishi maisha ya unyenyekevu na haki mbele ya Mungu wa kweli.

Habari hiyo pia inaonyesha kwamba Mungu aliwaangalia watu kama hao kwa neema yake kubwa, akiyaongoza mambo yao ya kila siku na kuwafanikisha. Wema huo pia ulikuwa baraka kwa taifa zima.

Tazama piaEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ruthu kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.