Steve Wembi

Mtaalam wa uhalifu na mwandishi wa habari


Steve Wembi (alizaliwa Kindu, Mkoa wa Maniema huko Zaire, sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, 20 Julai 1984) ni mtaalam wa uhalifu na mwandishi wa habari za uchunguzi anayeishi Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Nairobi, Kenya. Amefanya kazi kama mchangiaji wa New York Times, Al Jazeera na Xinhua. Yeye ni Mkurugenzi wa shirika la mawasiliano Consulting Media Agency (CMA).[1][2]

Steve Wembi
Amezaliwa (1984-07-20)20 Julai 1984
Kindu, Maniema, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Kazi yake mtaalam wa uhalifu, mwandishi wa habari
Miaka ya kazi 2007- sasa

Wasifu

hariri

Utoto na elimu

hariri

Steve Wembi alipita utoto wake huko Kalemie kaskazini mwa jimbo la Katanga. Mwaka 1997, yeye alifanyiwa mafunzo ya kijeshi uko Kamalenge wakati kuingia ya uasi AFDL wakiongozwa na Laurent Kabila kabla ya kurejea sekondari katika Taasisi ya Ibanda huko Bukavu, katika mkoa wa Kivu Kusini.[1]

Mnamo 2007, alihamia Kinshasa kuendeleza masomo yake ya chuo kikuu, miaka miwili katika Chuo Kikuu cha Kinshasa katika Kitivo cha Sheria. Yeye ana diploma katika jinai wa Taasisi ya Kenya Institute of Security and Criminal Justice. Tangu Julai 27, 2019, amekuwa mshauri wa mawasiliano kwa Alexis Thambwe-Mwamba, rais wa Seneti ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.[3][1]

Kazi ya media

hariri

Steve Wembi alianza, akiwa Chuo Kikuu cha Kinshasa, kazi yake ya uandishi wa habari kama mwandishi wa Xinhua katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mnamo 2007 huko Kinshasa ambapo alifanya kazi kwa media hii ya Wachina kwa miaka kumi.[4] Amefanya kazi kama mtayarishaji kweye televisheni na wavuti ya Al Jazeera,[5] CNN; na kama mwandishi wa shirika la habari la Umoja wa Mataifa Mtandao wa Habari za Kieneo (IRIN), jarida la The Economist, Financial Times, televisheni ya NRK ya Norwei na Jarida la The Wall Street Journal.

Katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Steve Wembi alishughulikia maasi kadhaa, pamoja na yale ya M23[6] na CNDP; lakini pia, alitembelea maeneo haswa huko Kasai,[7] mkoa ambao wataalam wawili wa UN Zaida Catalan na Michael Sharp waliuawa mnamo Machi 2017.[8] Mwaka huo huo, aligundua makaburi zaidi ya mia katika eneo la Ngaza. Baada ya uchunguzi na mashahidi kadhaa kutoka Kasaï, ambao walimfunulia habari juu ya mauaji ya wataalam hawa wawili, alichapisha kitabu "Ce que j'ai vu et entendu au Kasai".[9]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 "Biographie de Steve Wembi sur Muck Rack" Archived 14 Mei 2021 at the Wayback Machine., MackRack.Com (Consulté le 21 décembre 2020).
  2. "«Congo in Conversation» de Finbarr O’Reilly, lauréat du prix Carmignac", Radio France Internationale, 28 Avril 2020 (Consulté le 21 décembre 2020).
  3. "PRÉTENDUE DÉMISSION DU PRÉSIDENT DU SÉNAT : STEVE WEMBI DÉMENT CETTE RUMEUR" Archived 14 Mei 2021 at the Wayback Machine., Editeur.CD, 16 décembre 2020 (Consulté le 21 décembre 2020).
  4. "Congo in conversation" Archived 21 Desemba 2020 at the Wayback Machine., Afrique Invisu, 14 décembre 2020 (Consulté le 21 décembre 2020).
  5. "Beni, DRC: ‘They hacked him and threw him in a pigsty’", Al Jazeera, 29 aout 2016 (Consulté le 21 décembre 2020).
  6. "Ugandan Rebel Group Massacres 22 in Congo", New York Times, 08 octobre 2017 (Consulté le 21 décembre 2020).
  7. "ISIS Claims First Attack in the Democratic Republic of Congo", New York Times, 19 Avril 2019 (Consulté le 21 décembre 2020).
  8. "Congo Reports Arrest in Killing of 2 U.N. Experts", New York Times, 30 décembre 2017 (Consulté le 21 décembre 2020).
  9. "Le 11ème Prix du photojournalisme sur la RDC décerné à FinbarrO’Reilly" Archived 23 Septemba 2021 at the Wayback Machine., Le Potentiel, 29 avril 2020 (Consulté le 21 décembre 2020).

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Steve Wembi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.