10°09′32″S 19°57′45″E / 10.1590°S 19.9626°E / -10.1590; 19.9626


Mahali pa Sudi kati ya Lindi na Mtwara
Ramani ya Sudi (Ssudi) wakati wa ukoloni wa Kijerumani

Sudi ni kata ya Wilaya ya Mtama katika Mkoa wa Lindi, Tanzania.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 8,127 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 5,544 walioishi humo [2].

Msimbo wa posta ni 65202.

Eneo na historia

hariri

Sudi iko kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi kati ya Lindi na Mikindani-Mtwara, sehemu ambapo Mto Mambi unaishia baharini kwa mdomo mpana ambao ni hifadhi nzuri kwa jahazi.

Kabla ya ukoloni na wakati wa utawala wa Kijerumani ilikuwa moja ya bandari za maana kwenye mwambao wa kusini mwa Tanzania ya leo. Inasemekana iliundwa na Mwarabu tajiri aliyefanya biashara huko.

Mnamo mwaka 1900 ilikuwa na wakazi 2,000, mfanyabiashara mkuu akiwa Mohamed Chamdu [3].

Wajerumani waliunda hapa ofisi ya forodha. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Sudi ilikuwa kituo muhimu cha kijeshi cha Wajerumani; meli zilizoleta ramia na mahitaji ya kijeshi ziliweza kujificha katika hori ya Sudi inayofanywa na mdomo mpana wa Mto Mambi. Kwenye Septemba 1916 Sudi ilivamiwa na Waingereza[4].

Marejeo

hariri
  1. https://www.nbs.go.tz/
  2. http://www.meac.go.tz/sites/default/files/Statistics/Tanzania%20Population%20Census%202012.pdf Archived 3 Machi 2016 at the Wayback Machine. Sensa ya 2012, Lindi - Lindi DC]
  3. Kolonialhandbuch 1903, uk. 253
  4. Lochner, uk. 356

Vitabu

hariri
  • Rudolf Fitzner: Deutsches Kolonial-Handbuch, Band 1, toleo la 8, Berlin 1908, *Rochus Schmidt: Deutschlands Kolonien. Band 1, Berlin: Verlag des Vereins der Bücherfreunde Schall & Grund, 1898 (Reprint na Weltbild Verlag, Augsburg 1998, ISBN 3-8289-0301-0)
  • Reinhard K. Lochner: Kampf im Rufiji-Delta. München, 1987, S. 356, ISBN 3-453-02420-6
  • Makala "Ssudi", katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani (Deutsches Kolonial-Lexikon / ed. Heinrich Schnee. - Leipzig : Quelle & Meyer 1920. - Vitabu 3,) online hapa Archived 9 Desemba 2008 at the Wayback Machine.

Marejeo

hariri
  Kata za Wilaya ya Mtama - Tanzania  

Chiponda | Kiwalala | Longa | Majengo | Mandwanga | Mnara | Mnolela | Mtama | Mtua | Mtumbya | Nachunyu | Nahukahuka | Namangale | Namupa | Navanga | Nyangamara | Nyangao | Nyengedi | Pangatena | Sudi


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sudi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.