Shaheed Sukhdev Thapar (15 Mei 190823 Machi 1931) alikuwa mwanamapinduzi nchini Uhindi wakati wa utawala wa kikoloni wa Uingereza. Alikuwa mwanachama wa ngazi ya juu wa chama cha Hindustan Socialist Republican Association, alishiriki katika mashambulizi dhidi ya taasisi za serikali ya kikoloni chini ya Bhagat Singh na Shivaram Rajguru. Baada ya kumwua afisa wa juu wa polisi na kushiriki katika mashambulio ya kigaidi alipotega mabomu mahali mbalimbali alikamatwa na kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa tarehe 23 Mach1 1931 akiwa na umri wa miaka 23.

Sukhdev Thapar katika gazeti liloandika habari ya hukumu yao

Maisha ya awali hariri

Sukhdev Thapar alizaliwa Ludhiana, katika jimbo la Punjab nchini India tarehe 15 Mei 1908, wazazi wake wakiwa Ramlal Thapar na mama yake Ralli Devi.[1]. Baada ya kifo cha baba yake alichukuliwa na kulelewa na mjomba wake [2]

Adhabu ya Kifo hariri

Mnamo tarehe 23 Machi 1931, Thapar pamoja na wenzake wawili, Bhagat Singh na Shivam Rajguru, walinyongwa katika gereza la Lahore na miili yao ilichomwa moto kando ya mto Sutlej kufuatana na desturi ya Kihindu.

Marejeo hariri

  1. "Mark of a martyr - Sukhdev Thapar", The Tribune India, 13 May 2007. 
  2. Pramod Maruti Mande (2005). Sacred offerings into the flames of freedom. Vande Mataram Foundation. p. 251. ISBN 978-81-902774-0-2. 
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sukhdev Thapar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.