Turibio wa Mongrovejo

Turibio wa Mongrovejo (16 Novemba 153823 Machi 1606) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki nchini Peru.

Toribio Alfonso de Mogrovejo.

Ametambuliwa kuwa mtakatifu.

Tarehe ya kifo chake, yaani 23 Machi ndiyo sikukuu yake[1].

MaishaEdit

Turibio wa Mongrovejo alizaliwa nchini Hispania mnamo mwaka 1538.

Alijifunza sheria huko Salamanka, na mwaka 1580 aliteuliwa kuwa Askofu wa Lima nchini Peru, akaenda Amerika.

Alikuwa motomoto kwa kazi za kitume, akiitisha mikutano mbalimbali ili kurekebisha mambo ya dini katika nchi nzima.

Kwa nguvu zote alitetea haki za Kanisa, aliwatembelea Wakristo waliokuwa chini yake, na kufanya kazi kwa muda mrefu kwa mafaa ya wenyeji wa Peru.

Alifariki dunia mwaka 1606.

Tazama piaEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
  1. Martyrologium Romanum