Umbra
Umbra ni sehemu ya kivuli penye giza zaidi. Inaweza kuitwa pia kitovu cha kivuli.
Jina hilo hutumiwa hasa kutaja aina ya kivuli kinachotokea wakati wa kupatwa kwa Jua au kupatwa kwa Mwezi.
Umbra au kitovu cha kivuli hutofautishwa na penumbra au kivuli cha kando, ambako giza linapungua.
Wakati wa kupatwa kwa Jua umbra ni eneo jembamba la kilomita kadhaa ambako Jua linafunikwa kabisa na Mwezi ikiwa giza linatokea kwa dakika kadhaa wakati wa mchana.
Katika sehemu pana zaidi za penumbra au kivuli cha kando, Jua linaonekana kisehemu; karibu na kanda ya umbra mwanga unapungua lakini kwenye sehemu za nje ya penumbra tofauti ya mwanga ni ndogo.
Marejeo
hariri*[www.astronomy.ohio-state.edu/~pogge/Ast161/Unit2/eclipses.html Pogge, Richard "Lecture 9: Eclipses of the Sun & Moon"], Astronomy 161: An Introduction to Solar System Astronomy. Ohio State University. Imeangaliwa Mei 2021
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Umbra kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |