Veronika Giuliani

Veronika Giuliani alivyochorwa akiwa na alama zake maalumu.

Veronika Giuliani (Mercatello sul Metauro, Marche, Italia, 27 Desemba 1660 - Città di Castello, Umbria, Italia, 9 Julai 1727) alikuwa mmonaki wa urekebisho wa Wakapuchini wa Utawa wa Mt. Klara.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira. Ingawa aliheshimiwa hivyo mara baada ya kufa, kesi ya kumtangaza rasmi ilicheleweshwa na uchunguzi wa maandishi yake marefu.

Papa Pius VII alimtangaza mwenye heri mnamo Juni 1804, halafu Papa Gregori XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 26 Mei 1839.

MaishaEdit

Maandishi yake mwenyewe yanasimulia alivyoanza kujaliwa karama za pekee akiwa na umri wa miaka 3 tu, alipokuwa anaitwa Orsola.

Alijiunga na Waklara Wakapuchini wa monasteri ya Città di Castello mwaka 1667 ambapo akawa abesi tangu mwaka 1716 hadi kifo chake.

Kwa namna ya pekee aliambatana na Yesu msulubiwa kadiri ya karama ya Fransisko wa Asizi.

Kanisa Katoliki linakubali ukweli wa madonda matakatifu aliyosema alikuwanayo tangu tarehe 5 Aprili 1697 hadi kifo chake.

MaandishiEdit

Kwa agizo la padri aliyemuongoza kiroho, aliandika kirefu (kurasa 22,000 kwa mikono bila ya sahihisho lolote) kumbukumbu za maisha yake yote, ambazo zilitolewa baada ya kifo chake kwa jina Il Tesoro Nascosto (ni magombo 36).

Kutokana na shajara hiyo, Veronika Giuliani anahesabiwa kati ya Wakristo wanasala waliojaliwa mang'amuzi ya juu zaidi.

Tazama piaEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Veronika Giuliani kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.