Vinsenti wa Paulo

(Elekezwa kutoka Vincent wa Paulo)

Vinsenti wa Paulo (Pouy, Gascony, 24 Aprili 1581 - Paris, 27 Septemba 1660) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki kutoka [[Ufaransa] maarufu hasa kwa huruma yake kwa maskini na kama mwanzilishi wa mashirika mawili ya kitawa.

Mt. Vinsenti wa Paulo.

Akiwa amejaa roho ya kichungaji, huko Paris alijitosa kuhudumia fukara, akitambua sura ya Bwana Yesu katika sura ya kila mtu mwenye mateso akaanzisha Shirika la Misheni, halafu, akishirikiana na Luisa wa Marillac, lile la Mabinti wa Upendo, ili kufufua maisha ya Kanisa la mwanzoni, kulea kitakatifu wakleri na kusaidia maskini[1].

Miaka 1605-1607 alikuwa mtumwa wa Waislamu, kwanza nchini Tunisia, halafu Uturuki.

Alitangazwa na Papa Benedikto XIII kuwa mwenye heri tarehe 13 Agosti 1729, halafu Papa Klementi XII akamtangaza mtakatifu tarehe 16 Juni 1737.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • P. MYLES REARDEN, C.M., Mtakatifu Vinsent wa Paulo, Mhimiza wa Walei, Mlezi wa Masista, Mwalimu wa Mapadre – ed. Kitabu cha Kivinsenti – Mbinga 2000
  • A. RICHARTZ, Luisa wa Marillac, Mama asiye wa kawaida – tafsiri ya Masista wa Huruma wa Mt. Vinsenti wa Paulo – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1995 – ISBN 9976-67-095-8

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.