Anjelo wa Yerusalemu
Anjelo wa Yerusalemu, O.Carm. (Yerusalemu, leo Israeli/Palestina, 1185 – Licata, Sicilia, Italia, 1220) alikuwa mtawa na padri aliyefia dini.
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.
Maisha
haririAnjelo alizaliwa Yerusalemu katika familia ya Wayahudi.
Mama yake alipoongokea Ukristo, Anjelo alibatizwa pamoja na pacha wake, Yohane.[2] Baada ya wazazi wao kufariki mapema, mapacha hao walijiunga na utawa wa Wakarmeli wakiwa na umri wa miaka 18. Wakati huo walikwishaweza kuongea Kigiriki, Kilatini na Kiebrania.[2]
Alipofikia umri wa miaka 26 hivi, Anjelo alipewa upadrisho huko Yerusalemu, akaanza kusafiri nchi nzima. Alipoanza kujulikana kwa miujiza yake, alikimbilia makao ya upwekeni juu ya Mlima Karmeli.
Inasemekana huko alipata njozi iliyomuelekeza kwenda Italia akahubiri dhidi ya wazushi.[2]
Alipofika katika kisiwa cha Sicilia, umati wa watu ulimkimbilia ili kupata miujiza.
Alipojaribu kumuongoa mzushi Berengarius, aliuawa huko Licata, akifa siku 4 baada ya kupigwa, huku akiomba muuaji asamehewe.[2]
Heshima baada ya kifo
haririKaburi lake huko Licata likawa mahali pa hija.[2] Hatimaye Papa Pius II alithibitisha utakatifu wake.[2]
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
- ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 Sant' Angelo da Gerusalemme (di Sicilia)
Viungo vya nje
hariri- [1] Tovuti ya Wakarmeli
- (Kiitalia) Sant' Angelo da Gerusalemme (di Sicilia) Martire, carmelitano
- (Kiitalia) Santuario di Sant' Angelo da Gerusalemme (di Sicilia) Martire, carmelitano in Licata
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |