Joseph Smith
Joseph Smith, Mdogo (23 Desemba 1805 - 27 Juni 1844) alikuwa mwanzilishi na kiongozi wa Wamormoni.
Joseph Smith | |
Joseph Smith alivyochorwa. | |
Nchi | Marekani |
---|---|
Kazi yake | Wamormoni |
Mwaka wa 1827 alidai kuwa malaika alimtokea na kufunulia maagizo ya Mungu katika kitabu kipya, yaani Kitabu cha Mormoni. Mwaka wa 1830 alikichapisha kitabu hicho.
Miaka ya 1830, makao makuu ya Wamormoni yalianza jimboni Ohio, baadaye jimboni Missouri na kuanzia mwaka wa 1838 jimboni Illinois. Pale Smith Mdogo alitawala kama mwenyekiti wa kijiji mpaka alipouawa na umati wa watu wasiokubali utawala wake.
Alifuatwa kama kiongozi wa Wamormoni na Brigham Young aliyewaongoza Wamormoni kuhamia jimbo la Utah.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Joseph Smith kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |