Morogoro Vijijini

(Elekezwa kutoka Wilaya ya Morogoro vijijini)

Wilaya ya Morogoro Vijijini ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Morogoro nchini Tanzania yenye Postikodi namba 67200. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 263,920 [1].

Mahali pa Morogoro Vijijini katika mkoa wa Morogoro.

Ni wilaya yenye utajiri mkubwa wa hali ya hewa inayoruhusu mazao yote kustawi: kwa mfano, yale ya joto hustawi maeneo ya bondeni, na ya baridi sehemu za milimani. Ni chanzo cha mito inayonywesha mikoa ya Dar-es-Salaam na Pwani. Lakini asilimia kubwa ya wakulima hulima bila faida: hubeba mizigo kwenda sokoni kwa umbali mrefu zaidi ya kilometa 25.

Ni wilaya ya giza, ukiachia Ngerengere jeshini, kulikobaki hakuna lami wala umeme.

Shule zina upungufu mkubwa wa walimu.

Makabila ya wilaya hii ni Waluguru, Wabati, Wakutu, Wandengereko na mengine kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania: Waha, Wasukuma na Wanyaturu.

Morogoro vijijini kuna vijiji vingi vikiwemo Matombo, Mvuha na Kisaki ambavyo vina maliasili nyingi, ikiwemo misitu na maliasili nyinginezo.

MarejeoEdit

  Kata za Wilaya ya Morogoro Vijijini - Mkoa wa Morogoro - Tanzania  

Bungu | Bwakila Chini | Bwakila Juu | Gwata | Kasanga | Kibogwa | Kibuko | Kibungo Juu | Kidugalo | Kinole | Kiroka | Kisaki | Kisemu | Kolero | Konde (Morogoro) | Lundi | Matuli | Mikese | Mkambalani | Mkulazi | Mkuyuni | Mngazi | Mtombozi | Mvuha | Ngerengere | Selembala | Singisa | Tawa | Tegetero | Tomondo | Tununguo