Waraka wa Yakobo

(Elekezwa kutoka Yak)
Agano Jipya

Waraka wa Yakobo ni kati ya vitabu 27 vinavyounda Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mazingira

hariri

Kitabu hiki labda kiliandikwa miaka ya 80 B.K. kikitumia jina la Yakobo, lakini wataalamu hawapatani kuhusu huyo ni nani, aliandika wapi na lini.

Kwa hakika walengwa wa kitabu ni Wakristo wa Kiyahudi wenzake, lakini si barua halisi, bali ni mchanganyiko wa mawaidha yanayofuata mtindo wa vitabu vya hekima vya Agano la Kale lakini ujumbe wake ni kama mwangwi wa hotuba ya mlimani ya Yesu.

Lengo lake ni kuhakikisha Ukristo usiishie katika mawazo mazuri, bali imani ijitokeze katika matendo mema.

Lengo lingine ni kuwakuza mafukara na kuwakemea matajiri, kadiri ya mwelekeo wa Kanisa la Yerusalemu (Yak 1:1-2:26; 4:1-5:6).

Kiungo cha nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waraka wa Yakobo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.