Yesu kuzaliwa na Bikira

Yesu kuzaliwa na Bikira ni fundisho la imani linalosema kuwa Yesu Kristo alitungwa tumboni mwa mama yake, Bikira Maria, kwa uwezo wa Mungu (Roho Mtakatifu) tu, na kuwa Maria alipomzaa alikuwa bado bikira.

Maria "Kupashwa Habari" kadiri ya Guido Reni, 1621.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Katika Biblia ya Kikristo fundisho hilo linapatikana katika Injili mbili zilizo tofauti hata kwa vyanzo katika uzazi na utoto wa Yesu: Math 1:18-25[1] na Lk 1:26-38[2].

Mathayo anathibitisha hilo kwa kutaja utabiri wa maneno ya Isa 7:14 katika tafsiri ya Kigiriki ya Septuaginta: "Tazama bikira atachukua mimba, naye atazaa mwana, nao watamwita jina lake Emmanuel, yaani Mungu pamoja nasi".[3] [4]

Fundisho hilo linashikiliwa na madhehebu karibu yote ya Ukristo, hasa Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki.

Hata Waislamu wanakubali fundisho hilo kutokana na Kurani, hasa sura 3 (Al Imran) na 19 (Maryam (sura)).[5]

Tofauti na mafundisho mengine

hariri

Mara nyingine fundisho hilo linachanganywa na mengine tofauti,[6] kama vile utakatifu usio na doa wa Maria[7][8]na ubikira wa kudumu aliokuwa nao maisha yake yote[9]

Tanbihi

hariri
  1. 1:18Basi, hivi ndivyo Yesu Kristo alivyozaliwa: Maria, mama yake, alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla hawajakaa pamoja kama mume na mke, alionekana kuwa mja mzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. 19 Yosefu, mumewe, kwa vile alikuwa mwadilifu, hakutaka kumwaibisha hadharani; hivyo alikusudia kumwacha kwa siri. 20 Alipokuwa bado anawaza jambo hilo, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akamwambia, "Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, maana amekuwa mja mzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. 21 Atajifungua mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu, kwa kuwa yeye atawaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao." 22 Basi, haya yote yalitukia ili litimie lile neno Bwana alilosema kwa njia ya nabii: 23 "Bikira atachukua mimba, atamzaa mtoto wa kiume, naye ataitwa Emanueli" (maana yake, "Mungu yu pamoja nasi"). 24 Hivyo, Yosefu alipoamka usingizini alifanya kama malaika huyo alivyomwambia, akamchukua mke wake nyumbani. 25 Lakini hakumjua kamwe kimwili hata Maria alipojifungua mtoto wa kiume. Naye Yosefu akampa jina Yesu.
  2. 1:26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, "Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe." 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, "Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho." 34 Maria akamjibu, "Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?" 35 Malaika akamjibu, "Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. 36 Ujue pia kwamba hata Elisabeti, jamaa yako, naye amepata mimba ingawa ni mzee, na sasa ni mwezi wa sita kwake yeye ambaye watu walimfahamu kuwa tasa. 37 Kwa maana hakuna jambo lisilowezekana kwa Mungu." 38 Maria akasema, "Mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe kama ulivyosema." Kisha yule malaika akaenda zake.
  3. Brown, Raymond E.; Achtemeier, Paul J. (1978). Mary in the New Testament: A Collaborative Assessment by Protestant and Roman Catholic Scholars. Paulist Press. p. 92. ISBN 0-8091-2168-9.
  4. Diarmaid MacCulloch, A History of Christianity, 2009 (Penguin 2010, p. 81). ISBN 978-0-14-102189-8
  5. Sarker, Abraham.Understand My Muslim People. 2004 ISBN 1-59498-002-0 page 260
  6. O'Brien, Catherine (2012). The Celluloid Madonna. Columbia University Press. ISBN 978-0-23150181-1. Iliwekwa mnamo 22 Julai 2013.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. McKnight, Scot (2004). The Jesus Creed. Paraclete Press. uk. 301. ISBN 978-1-55725400-9. Iliwekwa mnamo 22 Julai 2013.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Harrington, S.J.J. (2010). Historical Dictionary of Jesus. Scarecrow Press. uk. 167. ISBN 978-0-81087668-2. Iliwekwa mnamo 22 Julai 2013.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Brown, Raymond Edward, mhr. (1978). Mary in the New Testament. Paulist Press. uk. 273. ISBN 9780809121687.

Marejeo

hariri

Marejeo mengine

hariri
  • Gromacki, Robert G. The Virgin Birth: Doctrine of Deity. Grand Rapids, Mich.: Baker Book House, 1981, cop. 1974. 202 p. ISBN 0-89010-3765-4
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yesu kuzaliwa na Bikira kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.