Yohane Payne

Yohane Payne (Peterborough, 1532Chelmsford, 2 Aprili 1582) alikuwa padri wa Uingereza aliyeuawa kwa ajili ya imani Katoliki wakati wa dhuluma za serikali ya nchi hiyo yenye Ushirika wa Anglikana kama dini rasmi.

Picha takatifu ya Mt. Yohane Payne.

Mwaka 1574 alijiunga na seminari huko Douai, Ufaransa, na miaka miwili baadaye alipata upadrisho[1]. Siku chache baadaye akarudi Uingereza pamoja na Cuthbert Mayne ili kufanya utume.

Alipokamatwa mara ya kwanza alilazimika kurudi Ufaransa, lakini mwaka 1579 alirudi tena Uingereza akafanya utume kwa mwaka mmoja unusu tena halafu alinyongwa kwa kisingizio cha usaliti dhidi ya malkia Elizabeti I; watu waliohudhuria walifaulu kuzuia asiraruliwe vipandevipande [2] kama mapadri wengine [3].

Alitangazwa mwenye heri na Papa Leo XIII tarehe 29 Desemba 1886 na mtakatifu na Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970[4].

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe 2 Aprili[5].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

MarejeoEdit

The most reliable compact source is Godfrey Anstruther, Seminary Priests, St Edmund's College, Ware, vol. 1, 1968, pp. 133–134, 311–313.

Viungo vya njeEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.