Yohane wa Misri

(Elekezwa kutoka Yohane wa Asyut)

Yohane wa Misri (kwa Kilatini: Iohannes anchorita, Yohane mkaapweke; 300 hivi - Asyut, 394), alikuwa mmonaki katika jangwa la Nitria (kwa Kiarabu: Wadi El Natrun; kwa Kigiriki: Sketis, Skete; kwa Kiingereza pia: Scetis).

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa hasa tarehe 17 Oktoba[1].

Maisha

hariri

Kisha kuwa seremala, Yohane aliacha kazi akatawa upwekeni kufuatana na wito kutoka kwa Mungu.

Baadaye alijitenga zaidi kwa kwenda kuishi juu ya kilele cha genge fulani.

Yohane alijulikana kwa juhudi zake za kufuata sauti ya Roho Mtakatifu hata alipodaiwa kufanya mambo yasiyo na maana ya kueleweka, kama kusogezasogeza miamba au kumwagilia miti iliyokauka.

Alikwepa hasa kuona wanawake ili asipatwe na vishawishi, lakini miaka 50 ya mwisho ya maisha yake alikwepa watu wote.

Augustino wa Hippo aliandika kuwa Yohane alishawishiwa na mashetani na aliponya watu kimuujiza, kwa mfano mwanamke kipofu.

Mbali ya dalili nyingi za uadilifu, alikuwa na karama ya unabii pia [2] na alisema na watu mara mbili kwa wiki kupitia dirishani, akionyesha pengine kuna anajua siri zao na kuwatabiria yajayo, kwa mfano ushindi wa Theodosius Mkuu.

Yohane alisali mfululizo, na siku tatu za mwisho aliacha hata kula na kunywa. Alipatikana maiti chumbani, akiwa katika mkao wa sala.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Butler, Alban. Lives of the Saints. Rock Island, Illinois: Tan, 1955.
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.