Alvaro Morata
Álvaro Borja Morata Martín, (kwa matamshi ya Kihispania: [alβaɾo moɾata]; alizaliwa Oktoba, 1992) ni mchezaji wa soka wa Hispania, anayecheza kama mshambuliaji wa Atletico Madrid kwa mkopo kutoka Klabu ya Uingereza na timu ya taifa ya Hispania.
Jinsia | mume |
---|---|
Nchi ya uraia | Hispania |
Nchi anayoitumikia | Hispania |
Jina katika lugha mama | Álvaro Morata |
Jina la kuzaliwa | Álvaro Borja Morata Martín |
Jina halisi | Álvaro |
Jina la familia | Morata |
Tarehe ya kuzaliwa | 23 Oktoba 1992 |
Mahali alipozaliwa | Madrid |
Lugha zinazozungumzwa, zilizoandikwa au zilizotiwa sahihi | Kihispania, Kiitalia |
Kazi | association football player |
Nafasi anayocheza kwenye timu | Forward (association football) |
Mwanachama wa timu ya michezo | A.C. Milan |
Medical condition | Unyogovu |
Mchezo | mpira wa miguu |
Namba ya Mchezaji | 7 |
Ameshiriki | UEFA Euro 2016 |
Kazi ya klabu
haririReal Madrid
haririAlianza kazi yake katika klabu ya Real Madrid, akicheza kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2010 na kuonekana katika michezo 52 rasmi madoli11, hasa kushinda Ligi ya Mabingwa mwaka 2014. [onesha uthibitisho]
Juventus
haririBaada ya kushinda Ligi ya Mabingwa mwaka 2014, alihamia Juventus kwa euro milioni 20 mwaka 2014, kushinda mara mbili ndani ya Serie A na Coppa Italia katika msimu wake wote kabla ya kununuliwa na Real madrid kwa mara nyingine kwa € 30,000,000.
Kurudi Real Madrid
haririMnamo tarehe 21 Juni 2016, Real Madrid ilimrejesha tena Morata kutoka katika klabu ya Juventus kwa € 30,000,000.Mechi yake ya kwanza ya ushindani ilikuwa mnamo tarehe 9 Agosti, na kushinda 3-2 dhidi ya Sevilla katika Kombe la Super Cup UEFA, na kubadilishana na Benzema baada ya dakika 62.G oli lake la kwanza alilipata katika mechi waliyoshinda 2-1 dhidi ya Celta Vigo mnamo Agosti 27.
Alishinda La Liga na Ligi ya Mabingwa mnamo mwaka 2016-17 kabla ya kujiunga na Chelsea mnamo mwaka 2017 kwa ada ya rekodi ya klabu ya karibu milioni 60. Mnamo Januari 2019, alihamia Atlético Madrid kwa mkopo na angejiunga na kilabu kabisa tarehe 1 Julai 2020.
Chelsea
haririMnamo tarehe 19 Julai 2017, Chelsea walitangaza kuwa wamekubaliana na Real Madrid kwa uhamisho wa Morata, kwa ada ya rekodi ya klabu ya £ 60 milioni. Mnamo tarehe 21 Julai, alifanikiwa kupitisha matibabu yake na rasmi akawa mchezaji wa klabu ya Chelsea.
Mnamo tarehe 5 Novemba 2017, Morata alifunga goli katika mechi ambayo walikuwa nyumbani dhidi ya Manchester United kwa goli1-0. Na katika mechi nyinine ambayo Chelsea walishinda 2-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika uwanja wa nyumbani Stamford Bridge.
Msimu wa 2018-19
haririMnamo 18 Agosti 2018, akifunga goli la pili katika ushindi wa nyumbani wa 3-2 dhidi ya Arsenal,Na pia Oktoba 4, alifunga goli katika ushindi wa 1-0 dhidi ya MOL Vidi katika hatua ya makundi katika UEFA Europa League.Mwezi mmoja baadaye, alifunga magoli mawili kusaidia kupata ushindi dhidi ya Crystal Palace kwa magoli 3-1 katika mechi ya ligi.
Atletico Madrid
haririMnamo tarehe 27 Januari 2019, Morata alirudi hispania katika klabu ya Atletico Madrid akijiunga na klabu kwa mkataba wa mkopo wa miezi 18.Alicheza katika ligi hiyo kwa mara ya kwanza mnamo Februari 3, katika mechi waliyokupoteza kwa kufungwa 0-1 mbali dhidi ya Real Betis.Alifunga goli lake la kwanza tarehe 24 Februari, katika ushindi wa nyumbani wa magoli 2-0 dhidi ya Villarreal.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Alvaro Morata kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |