Anselmi wa Lucca (pia: Anselmi wa Baggio; Milano, Italia, 1035 hivi; Mantova, Italia, 18 Machi 1086) alikuwa askofu wa mji huo baada ya somo na mtangulizi wake kuchaguliwa kuwa Papa Aleksanda II. Akiwa ndugu wa baba yake, huyo alimfanya kwanza kardinali (1062) ili amsaidie[1].

Mt. Anselmo.

Kabla ya hapo alipata elimu nzuri[2] na baadaye akawa mmonaki wa urekebisho wa Wabenedikto wa Cluny[3].

Aliungana na Mapapa mbalimbali kwa uaminifu mkubwa dhidi ya kaisari wa Ujerumani aliyetaka kuendelea kuingilia masuala ya Kanisa[4] na kwa ajili hiyo alidhulumiwa[5]. Hivyo alikabidhi mikononi mwa Papa Gregori VII pete na bakora alivyolazimishwa kuvipokea kutoka kwa kaisari Henri IV. Kisha kufukuzwa jimboni na wakanoni waliokataa kuishi naye kijumuia, alitumwa na Papa kama balozi huko Lombardia ambako aliweza kumsaidia sana.

Pia alishughulikia kukusanya sheria za Kanisa ili kusaidia urekebisho wa Kanisa lote [6]

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu[7] .

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Machi[8].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. This is according to Salvador Miranda.The Cardinals of the Holy Roman Church Archived 15 Januari 2020 at the Wayback Machine. Other sources consulted do not mention his promotion to the cardinalate. He is not listed among the cardinals of the 11th century in the modern printed prosopographies of the cardinals of that period (R. Hüls, Kardinäle, Klerus und Kirchen Roms: 1049–1130, Tübingen 1977; H.W. Klewitz, Reformpapsttum und Kardinalkolleg, Darmstadt 1957; K. Ganzer, Die entwicklung des auswärtigen Kardinalats im hohen Mittelater, Tübingen 1963)
  2. Fr. Alban Butler. "Saint Anselm, Bishop of Lucca, Confessor". Lives of the Fathers, Martyrs, and Principal Saints, 1866. CatholicSaints.Info. 17 March 2013. Web.
  3. Ott, Michael. "St. Anselm of Lucca, the Younger." The Catholic Encyclopedia. Vol. 1. New York: Robert Appleton Company, 1907. 10 Mar. 2015
  4. "Saint Anselm of Lucca". New Catholic Dictionary. CatholicSaints.Info. 30 July 2012
  5. Monks of Ramsgate. "Anselm of Lucca". Book of Saints, 1921. CatholicSaints.Info. 21 July 2012
  6. http://www.santiebeati.it/dettaglio/78150
  7. "Ansèlmo di Lucca, santo nell'Enciclopedia Treccani". www.treccani.it (kwa Kiitaliano). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-07-11. Iliwekwa mnamo 2019-07-11. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  8. Martyrologium Romanum

Marejeo

hariri
  • Mitrofanov, Andrey (2015). L'ecclésiologie d'Anselme de Lucques (1036–1086) au service de Grégoire VII: Genèse, contenu et impact de sa "Collection canonique". Instrumenta Patristica et Mediaevalia 69. Turnhout: Brepols Publishers. (ISBN|978-2-503-55489-1)
  • Cushing, Kathleen (1998). Papacy and Law in the Gregorian Revolution: The Canonistic Work of Anselm of Lucca. Oxford Historical Monographs. New York: Oxford University Press.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.