Bernardino wa Siena

Bernardino wa Siena (8 Septemba 1380 - 20 Mei 1444) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo na kasisi wa Kanisa Katoliki.

Pinturicchio (1486), Utukufu wa Mt. Bernardino da Siena, Roma, kanisa la Santa Maria in Aracoeli
Della confessione regole 12., 1494

Maisha ya awali hariri

 
Sancti Bernardini Senensis Opera omnia, 1745

Alizaliwa na kubatizwa Massa Marittima (Siena) tarehe 8 Septemba 1380 katika familia Albizzeschi kutoka Siena, ambako alihamia baada ya kubaki yatima, ili alelewe na kusomeshwa na ndugu zake.

Wito na utume hariri

Akiwa na umri wa miaka 22, alijiunga na utawa, katika tawi la urekebisho wa Waobservanti, ambalo akawa nguzo yake kuu, pamoja na Yohane wa Kapestrano, Yakobo wa Marka na Alberto wa Sarteano.

Kisha akaanza utume mkubwa akihubiri kwa mafanikio katika miji na vijiji vya Italia akivuta umati kwa maneno na mifano yake.

Kazi yake iliamsha katika Kanisa imani na ibada kwa Jina la Yesu na kurekebisha maadili ya wengi. Ndiye aliyesambaza kila mahali vibao vyenye kifupisho JHS (Jesus Hominum Salvator) kikiwa na msalaba juu yake na kuzungukwa na jua lenye miali 12[1].

Kifo hariri

Alifariki huko L'Aquila, tarehe 20 Mei 1444.

Heshima baada ya kifo hariri

Kutokana na sifa yake kubwa, alitangazwa mtakatifu na Papa Nikolasi V mwaka 1450.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 20 Mei[2].

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.