Christine Fellows
Christine Fellows (amezaliwa 1968) ni Mkanada mwimbaji na mwandishi wa nyimbo kutoka Winnipeg, Manitoba.[1] [2]
Historia
haririAmezaliwa Windsor, Ontario na kukulia Ufaransa na Kelowna, British Kolumbia. Fellows aliishi Toronto, Vancouver, Gulph na Montreal kabla ya kuhamia Winnipeg mwaka 1992.[3]
Mnamo 1992, aliunda kikundi chake cha kwanza, Helen, pamoja na Barry Mirochnick, Paul James, na Chang. Helen alijiengua mwaka 1995, na mwaka 1996 Fellows alijiunga na mwimbaji - mwandishi wa nyimbo Keri McTighe. Barry Mirochnick, Keith McLeod Peggy Messing, kuunda Special Fancy. Kundi lilitoa albamu moja, King Me.
Mnamo 2000 Fellows alitoa albamu yake ya kwanza, 2 Little Birds. Hii ilifuatiwa na The Last One Standing mwaka 2002, Paper Anniversary mwaka 2005, na Nevertheless mwaka 2007. Albamu hizi amewashirikisha Leanne Zacharias ("cello"), Jason Tait (ngoma, “vibraphone”), Barry Mirochnick (noma, sauti), John K. Samson (sauti, gitaa), Keith McLead (“mandolin”), Monica Guenter (“viola”), Greg Smith (besi), Ed Reifei (“percussion”) na Cristina Zacharias (violini).
Fellows ametumbuiza pamoja na Rheostatics, Veda Hille, The Mountain Goals, Kim Barlow, Martin Tielli, Old Man Ludecke na The Weakerthans. Ameolewa na kiongozi mwimbaji wa The Weakerthans, John K. Samson.[4]
Mnamo 2006, Fellows na Samson walirekodi The Old House, na albamu ilikuwa kama zawadi ya krismasi kwa marafiki na familia, ingawa walitoa nyimbo mbili, “Taps Reversed” na “Good Salvage”, kupigwa CBC Radio 3 mwaka 2007 mwanzoni. Fellows pia hutunga muziki kwa dansi, filamu, na televisheni.
Mnamo 2007, aliandika nyimbo kadhaa kwa ajili ya vipande vya dansi kuchezwa na mchezaji Susie Burpee; Baadae vilijumuishwa kwenye albamu yake binafsi, Nevertheless, ambayo ilitolewa 6 Novemba 2007. Fellows amefanya ziara kama mwanachama wa Pan-Canadian New Folk Ensemble pamoja na Kim Barlow na Old Man Luedecke,[5] na waga anashirikiana na msanii Shary Boyle. Alikuwa msanii mwenyeji katika Le Musée de Saint-Boniface Museum huko Winnipeg mwaka 2009.
Studio albamu yake ya tano, Femme de chez nous inajumuisha filamu / DVD ya onyesho mubashara ya Septemba 2009 Premiere of Reliquary/Reliquaire kazi aliyoitengeza kwa ajili ya makumbusho.[6]
Mnamo 2011, Samson, Fellows na Sandro Perri walishiriki kwenye Mradi wa Hifadhi za Taifa (National Parks Project ), akifanya kazi pamoja na mtayarishaji filamu Daniel Cockburn kutayarisha filamu fupi kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Bruce Peninsula (Bruce Peninsula National Park).[7] Pia alikuwa mbunifu wa sauti kwa "documentary" ya tovuti God’s Lake Narrows ya bodi ya taifa ya filamu ya Kanada (National Film Board of Canada).[8]
Albamu yake ya mwaka 2014 Burning Daylight ilitolewa kwa pamoja na mkusanyiko wa ushairi wa jina lile lile.[9]
Kwa sasa ni profesa msaidizi wa programu za uandishi bunifu za chuo cha British Kolumbia (University of British Columbia).
Hivi karibuni, Samsoni, Fellows, Ashley Au na Jason Tait walishirikiana katika muziki kwa For the Turnstiles, onyesho la dansi na kundi la Winnipeg Contemporary Dancers waliohamasishwa na albamu ya On the Beach ya Neil Young ya mwaka 1974.[10]
Mnamo 2016, Fellows na Tit walishirikiana kutayarisha albamu binafsi mpya ya Samson Winter Wheat.[11]
Diskografia
hariri- 2000: 2 Little Birds (Endearing Records)
- 2002: The Last One Standing (Six Shooter)
- 2005: Paper Anniversary (albamu) (Six Shooter)
- 2007: [[Nevertheless (albamu) (Six Shooter)
- 2011: Femmes de chez nous (Six Shooter)
- 2014: Burning Daylight
- 2018: Roses on the Vine
Marejeo
hariri- ↑ https://www.allmusic.com/artist/christine-fellows-mn0000412977/biography
- ↑ http://www.artsforall.ca/index.php/AFA/article/christine_fellows
- ↑ https://www.last.fm/music/Christine+Fellows/+wiki
- ↑ "John K. Samson and Christine Fellows" Archived 28 Septemba 2011[Date mismatch] at the Wayback Machine. Discorder, 4 December 2009.
- ↑ "The Pan-Canadian New Folk Ensemble Fall Tour 2008" Vue Weekly, 23 October 2008.
- ↑ Christine Fellows
- ↑ "John K. Samson, Christine Fellows and Sandro Perri "Bruce Beckons" (National Parks Project) (video)" Archived 26 Novemba 2013[Date mismatch] at the Wayback Machine. Exclaim!, 17 May 2011.
- ↑ "Winnipeg artist Kevin Lee Burton shares surprising glimpse of his hometown", 25 June 2011. Retrieved on 12 January 2012.
- ↑ "Christine Fellows' latest work evolved from album to multimedia art project". Winnipeg Free Press, 23 September 2014.
- ↑ "John K. Samson Scores Neil Young-Inspired Project in Winnipeg". Exclaim!, 29 April 2015.
- ↑ "John K. Samson Returns with 'Winter Wheat' Solo LP, Shares New Single". Exclaim!, 15 August 2016.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Christine Fellows kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |