Dola Huru la Kongo
Dola Huru la Kongo (kwa Kifaransa: État indépendant du Congo, kwa Kiingereza: Congo Free State) lilikuwa jina la koloni kubwa katika Afrika ya Kati kutoka mwaka 1885 hadi 1908 na kitangulizi cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya leo. Ilikuwa inamilikiwa kibinafsi na mfalme Leopold II wa Ubelgiji ilhali haikuwa chini ya serikali ya Ubelgiji.
Leopold aliweza kujipatia utawala juu ya eneo hilo kwa kushawishi mataifa mengine ya Ulaya kwenye Mkutano wa Berlin wa 1885 juu ya Afrika kwamba alikuwa akihusika katika kazi ya uhisani na hakutaka kukusanya ushuru wa biashara. [1] Kupitia Ushirika wa Kimataifa wa Kongo (International Association of the Congo) aliweza kueneza madai yake juu ya sehemu kubwa ya Beseni la Kongo.
Tarehe 29 Mei 1885, baada ya Mkutano wa Berlin kufungwa, mfalme alitangaza kwamba alikuwa na mpango wa kuendeleza mradi wake kwa jina la Dola Huru la Kongo (Congo Free State), jina ambalo lilikuwa bado halijatumika katika Mkutano wa Berlin na ambalo lilichukua rasmi nafasi ya "Ushirika wa Kimataifa wa Kongo" mnamo 1 Agosti 1885. [2] [3] [4]
Dola Huru la Kongo liliendelea kisheria kama nchi tofauti na Ubelgiji, chini ya utawala binafsi wa Leopold II, ingawa hakutembelea dola lake kamwe. [5]
Dola hilo lilijumuisha eneo lote la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya leo kutoka 1885 hadi 1908, wakati serikali ya Ubelgiji ilipochukua utawala juu yake badala ya mfalme. [6]
Utawala wa Leopold huko Kongo mwishowe ulipata sifa mbaya kwa sababu ya ukatili uliofanywa dhidi ya wenyeji. Dola la Leopold II lilivuna pembe za ndovu, mpira na madini katika bonde la juu la mto Kongo na kuviuza kwenye soko la Dunia kupitia makampuni ya kimataifa, ingawa kusudi lake kuu lilikuwa kuinua wenyeji na kuendeleza eneo hilo. Faida za kiuchumi zilipatikana kwa njia ya kazi ya kulazimishwa iliyopatikana kwa kutumia matishio na adhabu kali pamoja na kuua watu na kusababisha vifo kwa njaa.
Chini ya utawala wa Leopold II, Dola Huru la Kongo likawa moja ya kashfa kubwa zaidi za kimataifa kwenye mwanzo wa karne ya 20. Taarifa ya balozi mdogo wa Uingereza Roger Casement ilisababisha kukamatwa na kuadhibiwa kwa maafisa ambao walikuwa wamehusika na mauaji wakati wa kampeni ya kukusanya mpira mnamo 1903. [7]
Upotevu wa maisha na ukatili ulikuwa mandharinyuma ya riwaya mashuhuri ya "Heart_of_Darkness" ya Joseph Conrad. Kitabu chake pamoja na taarifa za magazeti na za wamisionari vilisababisha kilio cha kimataifa.
Wataalamu wanaendelea kujadiliana kuhusu idadi ya vifo katika kipindi hicho. [8] Makadirio ya juu zaidi yanasema kuwa mfumo wa kazi ya kulazimishwa ulisababisha moja kwa moja au kwa njia nyingine vifo vya asilimia 50 ya idadi ya watu katika koloni. [9] Inaaminiwa kwamba sehemu ya vifo zilisababishwa na ukatili wa maafisa ya koloni na sehemu nyingine pia na magonjwa mapya yaliyoletwa na Wazungu ambayo wenyeji walikosa bado kinga yake.
Wapinzani na wakosoaji wa hali ya Kongo waliendesha kampeni kubwa katika Ulaya na Marekani iliyosambaza habari ya matendo ya kinyama yaliyotokea. Mwandishi mwingine aliyesaidia sana kufichua mabaya alikuwa Arthur Conan Doyle, ambaye kitabu chake The Crime of the Congo kilisomwa sana kwenye mwanzo wa karne ya 20.
Kufikia mwaka wa 1908, shinikizo la umma na ujanja wa kidiplomasia ulisababisha kukomeshwa kwa utawala wa Leopold II katika Kongo. Makampuni makubwa yalishawishi pia serikali ya Ubelgiji kubadilisha utawala kwa sababu walitaka kuwekeza katika sekta ya migodi iliyolala tu wakati ule.
Hivyo Bunge la Ubelgiji lilitoa sheria iliyoweka utawala wa nchi katika mikono ya serikali.
Nchi ilijulikana baadaye kuwa Kongo ya Kibelgiji. Kwa kuongezea, kampuni kadhaa kuu za uwekezaji wa Ubelgiji zilishinikiza serikali ya Ubelgiji kuchukua Kongo na kuendeleza sekta ya madini kwani ilikuwa karibu haijashughulikiwa. [10]
Tanbihi
hariri- ↑ Gifford, Paul (1971). France and Britain in Africa. Imperial Rivalry and Colonial Rule. New Haven: Yale University Press. ku. 221–260. ISBN 9780300012897.
- ↑ Katzenellenbogen, S. (1996). "It didn't happen at Berlin: Politics, economics and ignorance in the setting of Africa's colonial boundaries.". In Nugent, P.; Asiwaju, A. I. (eds.). African Boundaries: Barriers, Conduits and Opportunities. London: Pinter. pp. 21–34.
- ↑ Cornelis, Sabine. 1991. "Stanley au service de Léopold II: La fondation de l'Etat Indépendant du Congo (1878-1885)". In H.M. Stanley: Explorateur au service du Roi, edited by Sabine Cornelis, 41-60. Tervuren: Royal Museum for Central Africa.
- ↑ Crowe, S.E. (1942). The Berlin West African Conference, 1884–1885. London: Longmans Green.
- ↑ MO - De koning in Kinshasa die nooit in Congo was [Slot]
- ↑ Britannica:"Congo Free State". Iliwekwa mnamo 22 Aprili 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Massacre in Congo State", January 5, 1900.
- ↑ "Being Colonized. The Kuba Experience in Rural Congo, 1880-1960", 2010.
- ↑ Hochschild, Adam (2006). King Leopold's Ghost: A Story of Greed, Terror, and Heroism in Colonial Africa. ku. 225–33. ISBN 978-1-74329-160-3.
- ↑ Gann, L.H. (1979). The rulers of Belgian Africa, 1884-1914. New Jersey: Princeton University Press. ISBN 9780691631813.
Vyanzo
hariri- ; also via HathiTrust
- Ó Síocháin, Séamas and Michael O’Sullivan, eds: The Eyes of Another Race: Roger Casement's Congo Report and 1903 Diary. University College Dublin Press, 2004. ISBN 1-900621-99-1.
- Stanley, Henry Morton, The Congo and the Founding of the Congo Free State (London, 1885)
- Report of the British Consul, Roger Casement, on the Administration of the Congo Free State, reprinted in full in The eyes of another race: Roger Casement’s Congo report and 1903 diary edited by Seamas O Siochain and Michael O’Sullivan. Dublin, 2003.
- The reports of the Congo Reform Association, particularly the "Memorial on the Present Phase of the Congo Question" (London, 1912).
- The Congo Report of Commission of Inquiry (New York, 1906)
- Burrows, Guy and Edgar Canisius, The Curse of Central Africa. London: Everett, 1903.
Viungo vya nje
hariri- Antwerp is a colonial city, by Bas De Roo
- Heart of Darkness, the novel
- The Crime of the Congo, by Sir Arthur Conan Doyle at Google Books
- A Journal of a Tour in the Congo Free State, 1905, by Marcus Dorman, from Project Gutenberg
- Catalogue of the Edmund Morel papers at the Archives Division of the London School of Economics.
- Archive Congo Free State, Royal museum of central Africa