Eugenius wa Karthago

Sanamu yake iliyoko Milano, Italia.

Eugenius wa Karthago (alifariki 13 Julai 505) alikuwa Mkristo aliyechaguliwa kwa kauli moja kuwa askofu wa Karthago mwaka 480 baada ya Deogratias wa Karthago (aliyefariki 456).

Ilimbidi apambane na Uario ulioungwa mkono na mfalme wa Wavandali ili kutetea imani sahihi. Alifaulu kuwavuta baadhi yao katika Kanisa Katoliki na kwa sababu hiyo alifukuzwa akaishi uhamishoni katika jangwa la Libia[1].

Baadaye aliruhusiwa kurudi, lakini miaka minane baadaye akafukuzwa tena ahamie Vienne, karibu na Albi (Ufaransa). Huko alijenga monasteri aliposhika maisha ya toba hadi kifo chake[2].

MaandishiEdit

  • Expositio Fidei Catholicae
  • Apologeticus pro Fide
  • Altercatio cum Arianis.[3]

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  1. On setting out he wrote a letter of consolation and exhortation to the faithful of Carthage which is still extant in the works of St. Gregory of Tours (P.L., LVII, 769-71)
  2. http://catholicsaints.info/saint-eugene-of-carthage/
  3. Cain, Andrew. “Miracles, Martyrs, and Arians: Gregory of Tours' Sources for His Account of the Vandal Kingdom.” Vigiliae Christianae, vol. 59, no. 4, 2005, pp. 412–437. JSTOR website Retrieved 13 July 2019.

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eugenius wa Karthago kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.