ESA ni kifupi cha Kiingereza cha "European Space Agency" (Mamlaka ya Usafiri wa Angani ya Ulaya). Taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 1975 na nchi 10 za Umoja wa Ulaya.

Mfano wa roketi ya Ariane 1 inayotumiwa na ESA
Kituo cha kusimamia operesheni kwenye anga-nje huko Darmstadt

Wajibu wake ni kuratibu miradi ya nchi za Ulaya ya kuendesha utafiti na uchunguzi wa anga. Shabaha ni hasa kuendeleza juhudi za nchi za Ulaya katika teknolojia ya angani iliyokuwa nyuma sana kulingana na kazi za Marekani na Urusi wakati ule.

Mwaka 2014 kulikuwa na nchi wanachama 20, na kati ya hizo kuna nchi 18 wanachama wa Umoja wa Ulaya pamoja na Uswisi na Norwei. Kufuatana na katiba yake, ESA inalenga shabaha zisizo za kijeshi pekee.

ESA inashirikiana kwa karibu na Umoja wa Ulaya na taasisi husika za kitaifa, hasa za Ufaransa na Ujerumani.

Katibu Mkuu wa ESA ni Mfaransa Jean-Jacques Dordain.

Ofisi na vituo vya EAS

ESA ina pia ofisi za mawasiliano katika Marekani, Urusi, Uingereza, Ufaransa na Ubelgiji. Mwaka 2013 kulikuwa na wafanyakazi wa ESA 2250.

Viungo vya nje

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: