Kalivari
Kalivari au Golgotha ni mahali mjini Yerusalemu panaposadikiwa Yesu alisulubiwa na kuzikwa.
majina hayo mawili yana maana moja: mahali pa fuvu la kichwa, ambapo paliitwa hivyo kutokana na sura ya mwinuko wake.
Jina la pili ni jina la Kiaramu lilivyotoholewa katika Kigiriki (Γολγοθᾶ[ς], Golgotha[s], kutoka golgolta; kwa Kiebrania gulgōleṯ), la kwanza ni tafsiri ya Kilatini (Calvariæ Locus, kutoka ufafanuzi wa neno asili uliotolewa na wainjili Marko na Mathayo: Κρανίου Τόπος, Kraníou Tópos).
Zamani za Uyahudi ya Kale na Roma ya Kale sehemu ya kuua wakosaji ilikuwa nje ya mji wenyewe. Injili ya Yohane 19:20 inaeleza mahali palikuwa "nje ya mji", yaani nje ya ukuta wa mji wakati ule. Waraka kwa Waebrania 13:12 unataja "nje ya lango" [1].
Mapokeo ya karne ya 3 yalisema ni ndani ya sehemu ambako Kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu lilijengwa, maana kufuatana na mapokeo hayo kaburi lilikuwa karibu na Golgotha. Leo hii eneo linapatikana ndani ya ukuta wa mji wa kale uliopo uliojengwa katika karne ya 16.
Tanbihi
hariri- ↑ Kigiriki asilia ni "ἔξω τῆς πύλης" ekso tes pyles, tafsiri ya Biblia Habari Njema inatumia "nje ya mji"
Viungo vya nje
hariri- Golgotha (Calvary) Hill-Photo: white stones, here visible right and left in the underground Archived 27 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
- The Hill of Calvary (Golgotha) shown in its original state Archived 19 Oktoba 2008 at the Wayback Machine.
- Location of Golgotha
- Web site for European Sacred Mountains, Calvaries and Devotional Complexes Archived 28 Novemba 2020 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kalivari kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |