Mtume Mathayo
Mathayo (kwa Kiebrania מַתִּתְיָהוּ, Mattityahu au מתי, Mattay, Zawadi ya Mungu; kwa Kigiriki Ματθαῖος, Matthaios) alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu anayeheshimiwa hasa kutokana na Injili yenye jina lake. Labda aliitwa pia Lawi.
Mitume wa Yesu |
---|
|
MaishaEdit
Kabla hajaitwa na Yesu Kristo amfuate, Mathayo alikuwa mtozaushuru, na kwa sababu hiyo alitazamwa na Wayahudi kama msaliti wa taifa na mkosefu.
Hata hivyo Yesu alipomkuta forodhani alimuambia, "Nifuate" (Injili ya Marko 2:14). Ndipo Mathayo akaacha vyote akaanza kuwa mwanafunzi wake. Katika nafasi hiyo alimuandalia karamu kubwa waliyoishiriki watozaushuru wengi, hata kusababisha lawama kwa Yesu toka kwa Mafarisayo.
Inasemekana kwamba baada ya ufufuko wa Yesu, Mathayo alieneza habari njema Ethiopia, ingawa masalia yake yanaheshimiwa huko Salerno (Italia) tangu mwaka 954.
MaandishiEdit
Kuna ushahidi wa zamani kwamba aliwahi kuandika misemo ya Yesu kwa lugha ya Kiaramu. Kitabu hicho kilipotea mapema, na ni vigumu kusema kina uhusiano gani na Injili ya Mathayo iliyoandikwa moja kwa moja kwa Kigiriki fasaha.
Heshima baada ya kifoEdit
Wakristo wa madhehebu yote wanamheshimu kama mtakatifu, hasa tarehe 21 Septemba[1] na 16 Novemba.
Anaheshimiwa kama msimamizi wa watu wa benki, forodha, watunzahesabu n.k.
Tazama piaEdit
TanbihiEdit
MarejeoEdit
- Thenashara, Mitume Kumi na Wawili – tafsiri ya P. A. Bunju – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1984 – ISBN 9976-63-030-1
Viungo vya njeEdit
- St Matthew the Apostle Archived 18 Novemba 2012 at the Wayback Machine. from The Golden Legend
- Apostle and Evangelist Matthew Orthodox icon and synaxarion
- Synaxis of the Holy Apostles
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtume Mathayo kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |