Grenada
Grenada ni nchi ya kisiwani kusini mwa Bahari ya Karibi. Iko kaskazini kwa Trinidad na Tobago na kusini kwa Saint Vincent.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Ever Conscious of God We Aspire, Build and Advance as One People | |||||
Wimbo wa taifa: Hail Grenada Wimbo la Kifalme: God Save the King | |||||
Mji mkuu | St. George's | ||||
Mji mkubwa nchini | St. George's | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza | ||||
Serikali | Ufalme wa kikatiba Bunge kwa namna ya Westminster Charles III Cécile La Grenade Keith Mitchell | ||||
Uhuru Kutoka Uingereza |
7 Februari 1974 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
344 km² (ya 203) 1.6 | ||||
Idadi ya watu - Julai 2012 kadirio - Msongamano wa watu |
109,590 (ya 185) 318.58/km² (ya 45) | ||||
Fedha | East Caribbean Dollar (XCD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-4) (UTC-4) | ||||
Intaneti TLD | .gd | ||||
Kodi ya simu | +1-473
- |
Ni nchi mwanachama wa jumuiya ya madola na mkuu wa Dola ni Mfalme Charles III wa Uingereza anayewakilishwa kisiwani na Gavana Mkuu.
Jiografia
haririEneo la nchi ni kisiwa kikuu cha Grenada pamoja na visiwa kadhaa za funguvisiwa ya Grenadini kama vile Carriacou, Petit Martinique, Rhonde Island na vingine vidogo.
Idadi kubwa ya wakazi iko Grenada penyewe pamoja na miji ya St. George's (mji mkuu), Grenville na Gouyave.
Visiwa vyote ni vya asili ya kivolkeno vyenye ardhi yenye rutuba. Grenada ina milima, na mkubwa zaidi ni mlima St. Catherine wenye kimo cha mita 840.
Watu
haririWakazi ni 110,000: walio wengi (82%) ni wa asili ya Afrika wametokana na watumwa waliopelekwa huko kulima mashamba ya miwa au ni machotara (13%) waliotokana na watumwa wale na mabwana wao Wafaransa. Waliobaki (5%) ni Wazungu na Wahindi. Wananchi walio wengi wanaishi nje: ni kama mara mbili kuliko waliobaki nchini.
Lugha rasmi ni Kiingereza, lakini walio wengi kwa kawaida wanaongea Krioli.
Upande wa dini, karibu wote ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (53%). Kati ya madhehebu ya Uprotestanti, wanaongoza Waanglikana.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Adkin, Mark. 1989. Urgent Fury: The Battle for Grenada: The Truth Behind the Largest U.S. Military Operation Since Vietnam. Trans-Atlantic Publications. ISBN 0-85052-023-1
- Beck, Robert J. 1993. The Grenada Invasion: Politics, Law, and Foreign Policy Decisionmaking. Boulder: Westview Press. ISBN 0-8133-8709-4
- Brizan, George 1984. Grenada Island of Conflict: From Amerindians to People's Revolution 1498–1979. London, Zed Books Ltd., publisher; Copyright, George Brizan, 1984.
- Martin, John Angus. 2007. A–Z of Grenada Heritage. Macmillan Caribbean.
- "Grenada Heritage". Grenadaheritage.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-05-10. Iliwekwa mnamo 2010-06-28.
- Sinclair, Norma. 2003. Grenada: Isle of Spice (Caribbean Guides). Interlink Publishing Group; 3rd edition. ISBN 0-333-96806-9
- Stark, James H. 1897. Stark's Guide-Book and History of Trinidad including Tobago, Grenada, and St. Vincent; also a trip up the Orinoco and a description of the great Venezuelan Pitch Lake. Boston, James H. Stark, publisher; London, Sampson Low, Marston & Company.
- Steele, Beverley A. 2003. Grenada: A History of Its People (Island Histories). MacMillan Caribbean. ISBN 0-333-93053-3
Viungo vya nje
hariri- Wikimedia Atlas of Grenada
- Official Website of the Government of Grenada
- Chief of State and Cabinet Members Ilihifadhiwa 10 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Grenada entry at The World Factbook
- Grenada Ilihifadhiwa 7 Juni 2008 kwenye Wayback Machine. at UCB Libraries GovPubs.
- Grenada katika Open Directory Project
- Grenada from the BBC News.
- Presentation Brothers College Ilihifadhiwa 20 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Key Development Forecasts for Grenada from International Futures.
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Grenada kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |