Ibaga ni kata ya Wilaya ya Mkalama katika Mkoa wa Singida, Tanzania, yenye msimbo wa posta 43509.

Kata ya Ibaga
Nchi Tanzania
Mkoa Singida
Wilaya Wilaya ya Mkalama
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 15,056

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa 15,056 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,712 waishio humo. [2]

Wakazi wa Ibaga kwa sasa ni wenyeji yaani Wanyisanzu, Wanyiramba na Wasukuma kwa kiasi kidogo na watu kutoka sehemu mbalimbali ambao ni mmojammoja.

Ibaga kwa sasa inakimbilia kuwa mamlaka ya mji mdogo kutokana na kuunganisha vijiji vya jirani kama Igengu, Mkiko, Kidaru, Tyegelo, Luono, Ndurumo, Mpambala, Lugongo, Nyahaa, Mkalama, Ilongo, Ilangida, Endasiku, Matongo, Isene, Nkinto, Mtamba, Kinyambuli na hata Mwangeza.

Maendeleo hariri

Pamoja na kuwa ni moja kati ya kata zinazounda tarafa ya Kirumi, Ibaga hapo kale ilijulikana kwa jina la utani Zaire Ndogo. Wakati huo ilikuwa na watu wengi waliotoka sehemu mbalimbali za nchi kuja kustaajabu na kujionea uwajibikaji uliokuwepo kwa kuwa ni kitovu cha biashara katika ukanda wa Iramba Mashariki.

Wakati huo kulikuwa na usafiri wa kutoka Ibaga kwenda Arusha hadi Mererani, wilaya ya Simanjiro, kwa ajili ya biashara na uchimbaji madini. Kwa sasa kuna usafiri wa mabasi kutoka Singida Ibaga hadi Meatu na Mwanza, Shinyanga, Maswa pamoja na usafiri wa mabasi kutoka Arusha hadi Ibaga.

Ibaga imerudi tena kuwa juu kutokana na uchumi kupanda kwa kasi: hii inatokana na biashara inayofanyika kati ya Mwanza, Arusha, Singida na Igunga.

Machimbo ya madini ya shaba yaliyopo Ilangida yameuongezea mji huu mdogo umaarufu, ingawa shaba, kwa mujibu wa kampuni kubwa zilizofanya utafiti, ipo chini sana, hivyo inahitaji mtaji mkubwa wa kuwekezwa ili uzalishaji uwe na tija.

Baada ya ugunduzi huo maisha ya hapa yamepanda: chakula na malazi vipo bei ghali, japo nyumba za wageni ni nzuri, zina mandhari safi, ambayo mtu kutoka mjini ataishi na kujisikia yupo bado mjini. Sehemu za kula starehe zipo kama baa ambapo kuna vinywaji baridi aina zote kwa bei rahisi.

Kituo cha polisi pamoja na mahakama vinahakikisha amani ipo masaa 24 siku 7 za wiki, hivyo ustawi wa mji huu unakwenda kwa kasi.

Tayari Ibaga ina miundombinu ya maji na umeme wa uhakika, huku ikielezwa kuwa, serikali ipo mbioni kuanza kujenga barabara kwa kiwango cha lami. Bado vijiji vichache sana hadi Juni 2023.

Kuna mnara wa Airtel, Zantel, Halotel na Vodacom.

Soko la Ibaga linapanuka hata kulishinda soko la mji kama Ndago. Kuna mnada wa kila mwezi ambao ni sikukuu ya kila tarehe mosi, pamoja na gurio maarufu kama lukule ya diwani kila siku ya jumamosi.

Ibaga ni kituo cha ununuzi wa mazao mbalimbali ya biashara kama karanga, ufuta, choroko, alizeti, mtama, uwele, mahindi n.k.

Kuna taasisi za elimu; shule mbili za msingi, yaani Kilimani na Ibaga, pamoja na sekondari ya kata ya Ibaga.

Katika masuala ya kijamii na kiutawala kuanzia mwaka 2015 kumekuwa na mwamko wa vijana kusaka fursa za uongozi kuanzia ngazi ya kijiji, kata, jimbo hadi taifa.

Uwepo wa kikundi maarufu cha ESAMA unaipa umaarufu wilaya ya Mkalama na Ibaga, kwani ndani ya kikundi hicho mna vijana wataalamu na wenye nia njema ya kuinyanyua wilaya.

Lakini pia uwepo wa vijana wasomi na wenye vipaji ni kichocheo kingine cha maendeleo kwa siku zijazo. Wamo vijana waandishi wa habari, watunzi wa riwaya na waandishi wa vitabu, akiwemo Joseph Shaluwa, akijulikana kama JOPASHA, ambaye, kwa kutumia kampuni yake, anasambaza vitabu vya shule za msingi, sekondari na dini.

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Mkalama - Mkoa wa Singida - Tanzania  

Gumanga | Ibaga | Iguguno | Ilunda | Kikhonda | Kinampundu | Kinyangiri | Matongo | Miganga | Mpambala | Msingi | Mwanga | Mwangeza | Nduguti | Nkalakala | Nkinto | Tumuli


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Singida bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ibaga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.