Kisiwa cha Krismasi

Territory of Christmas Island
Kisiwa cha Krismasi
Lugha rasmi Kiingereza, Kichina, Kimalay
Makao makuu Flying Fish Cove
Utawala Eneo la ng'ambo la Australia
Gavana Michael Jeffery
Pesa Dollar ya Australia
Wimbo wa taifa Advance Australia Fair
Karte der Weihnachtsinsel

Kisiwa cha Krismasi ni eneo dogo la Australia katika Bahari Hindi takriban km 500 upande wa kusini wa Jakarta, mji mkuu wa Indonesia, na 2,400 kaskazini kwa Australia yenyewe.

Kuna wakazi 1,600 wanokalia vijiji kaskazini mwa kisiwa. Theluthi mbili za eneo lake ni hifadhi ya taifa kwa sababu ya mazingira yake ya pekee pamoja na mimea na wanyama wake wasiopatikana mahali pengine duniani.

Jina na historia

hariri

Jina lake liliteuliwa kwa sababu nahodha Mwingereza William Mynors, aliyekuwa kati ya watu wa kwanza kuona kisiwa hicho, alifika huko siku ya Krismasi mwaka 1643. Wakati ule kisiwa kilikuwa bila watu.

Katika karne zilizofuata kisiwa kilitembelewa mara chache kwa sababu mwambao wake ni vigumu kukaribiwa kwa jahazi kubwa. Lakini baada ya kugunduliwa fosfeti kisiwani migodi ikaanzishwa na wafanyakazi kuhamia kutoka Singapur, China na Malaysia. Hao walikuwa mababu wa wenyeji wa leo.

Mwaka 1958 kisiwa kikakabidhiwa kwa Australia.

 
Kaa mwekundu ni mnyama wa pekee kisiwani.

Mazingira

hariri

Kisiwa cha Krismasi ni mahali pa pekee kwa sababu kinaonekana hakikufikiwa na watu hadi karne ya 16 na hakukaliwa nao hadi mwisho wa karne ya 19. Hivyo spishi nyingine zimehifadhiwa zilizoharibiwa penginepo.

Viungo vya Nje

hariri