Kisiwa cha Mafia
Mafia ni funguvisiwa la Tanzania, pamoja na jina la kisiwa kikubwa ndani yake, linalotazama mwambao wa Afrika ya Mashariki km 130 kusini kwa Dar es Salaam karibu na mdomo wa Mto Rufiji.
Kisiwa kikuu kina urefu wa km 49 na upana wa km 16; eneo lake ni takriban km² 400. Inajulikana pia kwa jina "Chole shamba" kutokana na mji wa kale wa Chole uliokuwepo kwenye kisiwa kidogo cha Chole kilichopo karibu na kisiwa kikuu kwa umbali wa mita 900.
WilayaEdit
Wilaya ya Mafia ni kati ya wilaya 6 za mkoa wa Pwani ikiwa na wakazi 40,801 (2002). Mji mkubwa na makao makuu ya wilaya ni Kilindoni.
Ina tarafa mbili ambazo ni:
- Tarafa ya kusini
- Tarafa ya kaskazini
Kata za wilaya ya Mafia ni kama zifuatazo:
Ina jumla ya vijiji 23.
UchumiEdit
Wakazi walio wengi ni wavuvi wanaolima pia mashamba madogo. Bidhaa za sokoni ni pamoja na nazi, chokaa na samaki.
Kuna utalii unaosifiwa sana lakini idadi ya wageni bado ni ndogo. Hasa Waitalia wamependa kutembelea Mafia pia kwa sababu ya jina la kisiwa ambalo kwa Kiitalia linamaanisha shirika la kigaidi lenye historia ndefu katika Italia ya kusini hadi siku ya leo.
HistoriaEdit
Mafia ilikuwa mahali pa miji ya kale ya utamaduni wa Waswahili kama vile miji ya Chole na Kua. Baada ya kuondoka kwa Wareno ilikuwa chini ya Sultani wa Omani (baadaye wa Zanzibar).
Mwaka 1892 Wajerumani walinunua Mafia kutoka kwa Sultani wa Zanzibar ikawa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani[1].
Mwaka 1915, wakati wa Vita Kuu ya Kwanza, Waingereza waliteka kisiwa wakishambulia kutoka hapa manowari ya Kijerumani ya SMS Königsberg mdomoni mwa mto Rufiji kutoka Mafia.[2]
Mnamo 1922, baada ya mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Mafia imekuwa sehemu ya Tanganyika, si tena Zanzibar.
Tazama piaEdit
TanbihiEdit
- ↑ Biashara hiyo iliwahi kukubaliwa mwaka 1890 katika Mkataba wa Helgoland-Zanzibar kati ya Uingereza na Ujerumani
- ↑ Mafia Island, German East Africa, January 1915, kuhusu uvamizi wa Mafia na Waingereza mwaka 1915, tovuti ya http://www.trenchfighter.homepage.t-online.de
Viungo vya njeEdit
- http://mafia-island-tanzania.gold.ac.uk/index_swahili.php Archived 23 Aprili 2009 at the Wayback Machine.
- Archaeology and History of Mafia Island Archived 21 Januari 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya Mafia Island Tanzania ya Pat Caplan
- Pat Caplan’s publications on Tanzania, hasa Mafia, in chronological order, as of 120411 Archived 23 Juni 2017 at the Wayback Machine.
- Asili ya Kua Archived 13 Aprili 2016 at the Wayback Machine., kuhusu historia ya mji wa Kua kisiwani Chole, ilivyokusanywa na Pat Caplan mnamo mwaka 1966
- Last Century in Mafia Island, blogu ya Mafiaisland.com
- Mafia kwa Geonames.org
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kisiwa cha Mafia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |