Magret Bays
Magret Bays (kwa Kifaransa: Marguerite; Sivierez, Fribourg, Uswisi, 8 Septemba 1815 – Sivierez, 27 Juni 1879), alikuwa mshonaji wa Uswisi.
Alijiunga na Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko na kutekeleza karama yake katika maisha ya nyumbani akijitosa kwa nguvu zote kusaidia wahitaji bila kuacha sala[1].
Mwaka 1854 alijikuta ana madonda mwilini kama yale ya Yesu msulubiwa. Pia alipata njozi.
Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 29 Oktoba 1995, halafu Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu tarehe 13 Oktoba 2019.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
haririViungo vya nje
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |