Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Idd ninga (majadiliano) 09:18, 19 Juni 2021 (UTC)Reply

Ndugu, asante na pongezi kwa kutunga makala nyingi, ila kabla hujaendelea soma vizuri maelekezo ya hapa juu. Kwanza kabisa usikubali tafsiri ya kompyuta bila kuipitia kwa makini ili kuhakikisha inaeleweka kweli. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:21, 25 Juni 2021 (UTC)Reply

Vyanzo

hariri

Salamu, tazama katika makala ya https://sw.wikipedia.org/wiki/Almami , uliweka vyanzo vinavyotokana na link za Wikipedia ya Kiingereza, vyanzo vya aina hiyo havikubaliki katika Wikipedia ya Kiswahili, tafuta vyanzo ambavyo havitokani na link za Wikipedia ya Kiingereza, Amani sana Idd ninga (majadiliano)

Kukuzuia

hariri

Kwa kuwa hujali maelekezo yetu, nakuzuia kwa wiki moja. Pole! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:19, 4 Agosti 2021 (UTC)Reply

Ndugu, kama hujaelewa kwa nini nimekuzuia kwa muda mfupi ni kwamba mimi na Iddi tumekupa maelekezo usiyafuate. Matokeo ni kwamba makala zako hazistahili katika Wikipedia, hasa kwa sababu ya tafsiri mbovu mno. Ila usikate tamaa, bali uwe tayari kupata masahihisho na maonyo. Sisi sote tumejifunza hivyo. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:32, 6 Agosti 2021 (UTC)Reply

Habari ndugu Riccardo Riccioni natumai muda wa adhabu ulionipa umeisha kwa sasa na kiukweli nimejifunzaa naaidi kua makini katika ufanyaji kazi wangu hivyo naomba unifungulie niendelee na kazi. Asante Awadhi Awampo (majadiliano) 08:34, 12 Agosti 2021 (UTC)Reply

Sawasawa, ila naona makala yako mpya kuhusu Amerika ya Kusini ina matatizo tayari. Uirekebishe kwa kufuata fomati inayotakiwa. Amani kwako! Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:03, 12 Agosti 2021 (UTC)Reply
Sawah lakini najitaidi sana kuto kufwata google translator ningependa kujuaa pia kuna makosa gani katika nakala iyo ya Amerika ya kusini uwenda kuna kitu sijakielewa vizuri Awadhi Awampo (majadiliano) 10:12, 12 Agosti 2021 (UTC)Reply
Kwanza hakuna utangulizi unaohusika moja kwa moja na kichwa. Pili vyanzo kutoka Wikipedia ya Kiingereza havikubaliki. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:15, 12 Agosti 2021 (UTC)Reply

Nimeifanyia marekebisho naomba kujua kama kuna makosa tenaa Awadhi Awampo (majadiliano) 10:42, 12 Agosti 2021 (UTC)Reply

Usahihishe makala zako kabla ya kuendelea!

hariri

Ndugu nimepitilia makala zako kadhaa. Leo umeanzisha VVU/KIMWI huko Armenia (ulikosea kuandika Ukimwi, uliandika "kimwi" tu). Yote ni tafsiri ya google (100%) lakini umejitahidi kusahihisha sehemu kubwa ya kasoro. Ila sentensi ya mwisho imetoka vibaya. Siwezi kukuzuia kufuata google translate lakini naweza kuchukua hatua nikiona hutaki au huwezi kuisahihisha iwe Kiswahili. -- Labda hujatambua bado lakini huwezi kufuata google kama sentensi za Kiingereza ni ndefu, matokeo yake kamwe ni Kiswahili (kama katika makala hiyo). Programu zina kasoro mbili A) zinachanganya maneno, ambayo ni rahisi kuona; B) zinapanga sentensi au maelezo kwa namna isiyolingana na lugha ya pili na kuzifanya hazieleweki. Hapo LAZIMA UTAFAKARI, washa bongo na andika sentensi inayoeleweka kwa bibi yako au mtoto wa miaka 6. Kata habari ya Kiingereza kwa sentensi 2 au tatu, usitumie tu maneno kwa tafsiri lakini tunga maelezo badala yake. Kama sentensi ya Kiingereza ina kitenzi mwishoni baada ya mfululizo wa maelezo lazima uiweke kwenye mwanzo.

Naona pia hujarudi kuangalia makala ulizowahi kutunga, mfano VVU/UKIMWI nchini Guinea, VVU / UKIMWI huko Amerika Kaskazini, VVU / UKIMWI huko Amerika ya Kusini. Ninakuonya sasa. Ilhali sasa umejitahidi, sikuzui sasa. Lakini naomba uniambie karibuni jinsi gani na lini unataka kushughulika kasoro katika makala zako za awali. Maana usiendelea kutunga mapya kabla ya kufanya usafi.

Kwa jumla makala zako zote zina kasoro katika muundo. 1) Huweki interwiki, wala 2) kichwa cha Marejeo / Tanbihi (ona Wikipedia:Mwongozo_(Kutaja_vyanzo). Pia hufuati taratibu wa kuonyesha maneno ya kwanza = lemma ya makala kwa herufi koze. 3) Viungo vya ndani unatumia mara chache mno. Kipala (majadiliano) 10:47, 12 Agosti 2021 (UTC)Reply

Pitia Mkala

hariri

Salamu, katika makala hii hapa ( https://sw.wikipedia.org/wiki/Mgomo_wa_watumishi_wa_umma_wa_Afrika_Kusini_mwaka_2007 ) kwanza makala imekuwa na kiswahili ambacho ni kigumu kueleweka hali ambayo inaweza kusababishwa kuwekewa alama ya tafsiri ya Kompyuta, pia makala haina interwiki hivyo, hivyo kuwa na ugumu zaidi wa kuweza kuipata makala katika lugha nyingine na kushindwa kuifanyia marekebisho, hebu pitia kwanza makala zako kabla ya kuendelea kuandika makala nyingine,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 22:47, 24 Agosti 2021 (UTC)Reply

Taarifa ya kukuzuia!

Ndugu, imenibidi kukuzuia kwa sababu zinazotajwa chini. Wakati unapokuwa umezuiwa huwezi kuhariri isipokuwa penye huu ukurasa wako wa majadiliano. Unaweza kunijibu kwa kutumia “Email this user”.

Sababu ni kuwa umeingiza matini iliyopatikana kwa njia ya tafsiri ya kompyuta ikiwa na kasoro nzito ya lugha. Umearifiwa kwamba ni marufuku kumwaga matokeo ya google translate katika makala zetu. Wachangiaji wanaopuuza utaratibu huu wanasababisha hasara kubwa kwa Wikipedia yetu na kuwapa wengine kazi kubwa mno ya kusafisha makosa yao.

Bila shaka una nia nzuri kuchangia katika Wikipedia. Tutafurahi kushirikiana nawe lakini ni lazima ufuate utaratibu. Kazi yetu kama wakabidhi ni kulinda mradi huu.

Ukiwa tayari kufuata utaratibu pamoja na kupitia upya matini ulizozileta tayari, naomba uwasiliane nami kwa kufungua ukurasa wangu (bofya jina langu chini) na kuniandikia baruapepe kwa kubofya “Email this user” upande wa kushoto. Hapo nitaweza kukuruhusu tena. Hapo lazima uwezeshe njia kwa kufuata maelezo katika Wikipedia:Email.

ona Mgomo wa watumishi wa umma wa Afrika Kusini mwaka 2007. Nimewahi kukuonya. Hujajibu. Wala hukujali. Basi. Kipala (majadiliano) 22:55, 24 Agosti 2021 (UTC)Reply

habari ndugu kipala nilikua naomba kufunguliwa akaunti yangu iliyofungwa tarehe 22 mwezi wa nane kutokana na makosa yakujirudia rudia. naahidi kubadilika kutokana na darasa nililolipata kupitia event iliyofanyika mkoani morogoro tarehe 20 mwez wa kumi na moja . Nimejifunza mambo mengi mapya na nimetambua sehemu ambazo nilikua nakosea katika ufanyaji kazi wangu pia ningependa kufunguliwa IP adress yangu ili kama kutakua na changamoto au makosa madogo madogo nipate msaada kwa wakati . natumai ombi langu litafanyiwa kazi asante. Awadhi Awampo (majadiliano) 10:13, 30 Novemba 2021 (UTC)Reply
habari ndugu kipala nilikua naomba kufunguliwa akaunti yangu iliyofungwa tarehe 22 mwezi wa nane kutokana na makosa ya kujirudia rudia. Naahidi kubadilika kutokana na darasa nililolipata kupitia event iliyofanyika mkoani morogoro tarehe 20 mwezi wa kumi na moja. Nimejifunza mambo mengi mapya kupitia event hiyo na nimetambua sehemu ambazo nilikua nakosea katika ufanyaji kazi wangu pia ningependa kufunguliwa IP adress yangu ili kama kutakua na changamoto au makosa madogo madogo niweze kupata msaada kwa wakati. natumai ombi langu litafanyiwa kazi Awadhi Awampo (majadiliano) 09:43, 2 Desemba 2021 (UTC)Reply
Asante naomba uwezeshe mawasiliano kwa email kwa kufuata maelezo hapo : Wikipedia:Email
Kipala (majadiliano)
10:22, 2 Desemba 2021 (UTC)Reply
Bado makala zako zina matatizo mbalimbali. Uwe makini zaidi! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:01, 25 Februari 2022 (UTC)Reply
sawa asante kwa taarifa . ningependa kujua seem ambazo bado ninakosea ili niweze kujirekebisha asante. Awadhi Awampo (majadiliano) 20:09, 25 Februari 2022 (UTC)Reply
Siwezi kukueleza makosa yote. Angalia mwenyewe nilivyorekebisha kwa kufungua ukurasa "Mabadiliko ya karibuni" na kutazama "tofauti" kati ya ukurasa ulivyotungwa na wewe na nilivyohariri mimi. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:14, 26 Februari 2022 (UTC)Reply

Vyanzo vya Kiingereza

hariri

Salamu, tazama katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Loubna_Abidar , kumbuka kwamba vyazo vya kiingerza katika makala ya Wikipedia ya Kiswahili havitakiwi, Zingatia hilo, pitia na urekebishe makala yako. Idd ninga (majadiliano) 12:20, 28 Februari 2022 (UTC)Reply

Onyo la Mwisho

hariri

Salamu Ndugu Awadhi, mara ya mwisho nilikutumia ujumbe katika ukurasa wako wa majadiliano hapo juu kuhusu kutumia vyanzo vinavyotokana na Makala za Kiingereza, lakini bado umekuwa ukiendelea kuleta makala za aina hiyo, tazama katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Latifa_Jbabdi , ni bora sasa kuacha kuweka vyanzo vya aina hiyo maana havina maana yeyote na pia inaonyesha kuwa haufuati utaratibu mzuri wa kuanza kaundika makala zako,REKEBISHA kabla ya Kuendelea,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 08:59, 1 Machi 2022 (UTC)Reply

salamu ndugu Idd Ninga katika kutumia vyanzo vya kiingereza katika makala ya Loubna Abidar nimebadilisha kwa kutafuta vyanzo tofauti vinavoendana na makala husika Awadhi Awampo (majadiliano) 09:21, 1 Machi 2022 (UTC)Reply
Asante kwa masahihisho sasa nimegundua nilipokua nakosea pia kama kuna kosa lolote nahitaji kujua ili niweze lifanyia marekebisho Awadhi Awampo (majadiliano) 10:23, 1 Machi 2022 (UTC)Reply

Interwiki

hariri

Habari! Kwa makala ambazo zina lugha zaidi ya moja, ni vizuri kuweka kiungo cha lugha nyingine (interwiki). Kujifunza zaidi soma hapa. Czeus25 Masele (majadiliano) 13:30, 3 Machi 2022 (UTC)Reply

asante ndugu Czeus25 Masele nitalifanyia kazi kwa kuongea na uongozi wangu vizuri ili nipate msaada katika mafunzo ya kuongeza lugha Awadhi Awampo (majadiliano) 19:07, 4 Machi 2022 (UTC)Reply
Kweli, jitahidi kuweka kiungo kwenda makala kama za kwako katika lugha nyingine. Pia angalia nilivyorekebisha ulivyoandika ili uzidi kupunguza makosa. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:30, 5 Machi 2022 (UTC)Reply

Maboresho

hariri

Jaribu kutumia muda mwingine kupitia makala zako za nyuma kuona maboresho yaliyofanyika ili uwezo kuyatumia katika makala zako mpya utakazo kuwa unaandika, Kumbuka kuweka alama ya Mbegu,katika makala zako,Ukipitia maboresho ya nyuma utaona jinsi makala zinavyoonekana tofauti na ulivyozianzisha, Amani Sana Idd ninga (majadiliano) 17:38, 21 Machi 2022 (UTC)Reply

asante kwa maelezo lakini ningeomba kuona tofauti ya makala nnazo hariri mimi na mnazo zilekebisha nizijue kwa majina angalau makala tano ili niweze kujifunza zaidi katika hilo asante Awadhi Awampo (majadiliano) 19:05, 21 Machi 2022 (UTC)Reply
alama ya mbegu inawekwa kama jamii inayojitegemea? Awadhi Awampo (majadiliano) 19:10, 21 Machi 2022 (UTC)Reply
Angalia walau kurasa mbili za mwisho ulizozitunga. Kuhusu mbegu, itajitokeza yenyewe katika jamii ukiandika vizuri, kwa mfano: {{mbegu}}, au {{mbegu-mtu}}, au {{mbegu-cheza-mpira}} au {{mbegu-igiza-filamu}}. Hivyo, usiandike: [[Jamii:Mbegu]] n.k. Pia usizidishe jamii bure. Kwa kawaida, ukiandika Jamii:Wanawake wa Tanzania, hakuna haja ya kuandika pia: Jamii:Wanawake na Jamii:Watu wa Tanzania. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:57, 22 Machi 2022 (UTC)Reply
asante kwa mafunzo mapya naahidi kulifanyia kazi Awadhi Awampo (majadiliano) 19:46, 22 Machi 2022 (UTC)Reply
ndugu Riccardo nimeweza kuhariri makala zifuatazo kwa kufuata utaratibu niliojifunza hapo juu hivyo naomba upitie makala hizi na kunisahihisha "https://sw.wikipedia.org/wiki/Halima_Rafat","https://sw.wikipedia.org/wiki/Rangina_Hamidi","https://sw.wikipedia.org/wiki/Massouda_Jalal". asante Awadhi Awampo (majadiliano) 06:41, 23 Machi 2022 (UTC)Reply
Habari!, naona bado unatumia , tafadhali soma vizuri maelekezo uliyopewa hapo juu utafanya vizuri. Ahsante. Czeus25 Masele (majadiliano) 08:10, 23 Machi 2022 (UTC)Reply

Zuio ?

hariri

Najiuliza kama ninapaswa kukuzuia tena. Baada ya kukagua makala za Frank Chester Robertson, Kundi la Algoa, naona bado unatumia google translate ukisahihisha kidogo tu. Lakini unaacha matini isiyoeleweka. Tena naona una tabia kuanzisha makala ambazo humalizi, ukiacha makala mafupi bila maudhui halisi baada ya kutafsiri mistari michache tu bila kujali makala inmasema nini. Ona Uuaji wa Abdirahman Abdi ambayo ni bure kabisa jinsi ilivyo. Kipala (majadiliano) 08:19, 21 Julai 2022 (UTC)Reply

habari ndugu kipala nimeweza kuzifanyia marekebisho makala ambazo zilikua na makosa hapo mwanzoni kwani zilikua ni makala za majaribio kwa mtumiaji mpya nilikua namuelekeza namna ya utendaji kazi wetu.
asante na naomba kama kuna tatizo nirekebishwe Awadhi Awampo (majadiliano) 20:21, 25 Julai 2022 (UTC)Reply

Hakiki Makala Zako

hariri

Ni bora sasa ukawa unapitia makala zako na kuzihakiki kabla ya kuchapisha, kwa sababu makala nyingi unaandika sehemu ya herufi kubwa unaweka herufi ndogo, na hiyo inatokea kwa maneno mengi katika makala moja, hivyo kuzalisha makala yenye makosa mengi ya kiuandishi, pia mwanzo wa jina la makala yako weka alama hii ((' ' ') badala ya kuweka alama nne au zaidi, hiyo hufanya maandishi yako kulala (kuwa na italic) na hivyo kuharibu muonekano mzuri wa makala zako, Amani sana, Idd ninga (majadiliano) 21:53, 7 Agosti 2022 (UTC)Reply

Awadhi Awampo (majadiliano) 06:41, 8 Agosti 2022 (UTC)Reply
Habari ndugu Awadhi, hongera kwakuitikia mashauri. Unaendelea kufanya vizuri hivo pitia marekebisho kidogo niliyo yafanya kwenye makala zako katika ukurasa wako wa mtumiaji na nyingine ulizoweka tayari ili uone wapi bado hujawa sawa. 1) Bado kwenye makosa ya kiuandishi (typos), 2) Maneno yanayo takiwa kuanza na Herufi kubwa, 3)kuto kuacha nafasi kati ya neno na neno 4) kutumia viunganishi vingi kupitiliza katika sentensi moja. Amani -- Olimasy (majadiliano)